Thursday, 13 August 2015

MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE CCM MAJIMBO YOTE YAMETOKA



Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo imetangaza majina ya wagombea ubunge, ubunge viti maalum, uwakilishi na uwakilishi viti maalum ambapo baadhi ya wagombea walioshinda kwenye kura za maoni wametupwa nje na kuchukuliwa mshindi wa tatu.





Akizungumza leo na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo yamelazimika kurudia kupiga kura za maoni na mengine kuhesabu upya kura zilizopigwa baada ya kujitokeza malalamiko kwa wagombea.

Amesema kuna baadhi ya majimbo ambayo wamelazimika kumchukua mshindi wa tatu kwenye kura za maoni na kuwaacha walioshinda nafasi ya kwanza na ya pili ili kumaliza migogoro iliyokuwepo.

Ameyataja majimbo 11 ambayo yatarudia uchaguzi wa kura za maoni kuwa ni Ukonga, Kiteto, Chilonwa, Kilolo, Njombe Kusini, Makete, Namtumbo, Rufiji, Mbinga Vijijini, Busega na Singida Mashariki.

Aidha Nnauye amesema kuwa uchaguzi wa viti maalum kupitia umoja wa wanawake Tanzania (UWT) yamepitishwa kama yalivyotoka mikoani ambapo ni mkoa mmoja tu wa Dar es Salaam ambao NEC imetengua ushindi wa mshindi wa kwanza, Angela Kiziga ambaye ni mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na badala yake aliyeshika nafasi ya pili na ya tatu ndiyo waliopitishwa katika ubunge wa viti maalum.


Waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM kwenye Majimbo ya mkoa wa Shinyanga ni:-

1.Shinyanga mjini-Ndugu Steven Masele
2.Solwa-Ndugu Ahmed Ally Salum
3.Kishapu-Ndugu Suleiman Masoud Nchambi
4.MsalalaNdugu Ezekiel Magolyo Maige
5.Ushetu-Ndugu  Elias John Kwandikwa 
6.Kahama Mjini-Ndugu Kishimba Jumanne Kibera


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!