Monday, 6 July 2015

YALIYOJIRI MAHAKAMANI KISUTU WAKATI WA KUSOMWA HUKUMU YA MAWAZIRI WA ZAMANI DANIEL YONA , BASIL MRAMBA NA AGREY MGONJA

Screen Shot 2015-07-06 at 4.24.26 PM

Kesi iliyokuwa inawakabili Basil Mramba, Daniel Yona na Agrey Mgonja kuhusu matumizi mabaya ya madaraka imetolewa hukumu leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.

Daniel Yona na Basil Mramba waehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya Milioni tano kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya makosa 11, Grey Mgonja ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia.
Screen Shot 2015-07-06 at 4.23.50 PM
Basil MrambaDaniel Yona na Grey Mgonja wakiwa nje ya mahakama ya Kisutu kusubiri kuingia ndani
Screen Shot 2015-07-06 at 4.23.59 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.24.06 PM
Familia ya Daniel Yona na Basil Mramba wakiingia Mahakamani
Screen Shot 2015-07-06 at 4.24.16 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.24.35 PM
Daniel Yona akiagana na rafiki zake
Screen Shot 2015-07-06 at 4.24.45 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.24.53 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.25.03 PM
Basil Mramba akiingia ndani ya Gari ya Polisi kuelekea gerezani.
Screen Shot 2015-07-06 at 4.25.14 PM
Daniel Yona akiingia ndani ya gari ya Polisi kuelekea Gerezani.
Screen Shot 2015-07-06 at 4.25.23 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.25.31 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.25.42 PM
Screen Shot 2015-07-06 at 4.25.50 PM
Gari ya polisi iliyobeba watuhumiwa ikitoka nje ya Mahakama ya Kisutu.

Ndugu wa Mramba akiangua kilio mara baada ya hukumu hiyo.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewahukumu kwenda jela miaka mitatu na kulipa faini ya milioni tano aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona huku ikimuachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja baada ya kumuona hana hatia.
Vigogo hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7
Hukumu hiyo imetolewa chini ya jopo la mahakimu watatu ambao ni Hakimu Saul Kinemela, Jaji Sam Rumanyika na Jaji John Utamwa aliyekuwa mwenyekiti wa jopo hilo baada ya kupitia ushahidi pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa na pande zote mbili katika kesi hiyo.
Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka 2008 wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
Katika utetezi wake, Mramba alikiri kuisamehe kodi kampuni hiyo kwa kuwa kulikuwa na mkataba uliosainiwa Juni 2003 kati ya kampuni hiyo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao ulikuwa unaonesha malipo yafanyike bila ya kukatwa kodi.
Mgonja alidai kuwa yeye ndiye aliyemshauri Mramba kuisamehe kodi kampuni hiyo kutokana na mkataba huo. Hata hivyo, inadaiwa msamaha wa kodi ulitolewa wakati tayari Wizara ilikuwa imepokea barua za kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo zilikuwa zinakataza kampuni hiyo isisamehewe kodi.

KWA HISANI YA MILLARD AYO.COM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!