Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, (kushoto) akipokea fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa Singida kutoka kwa Katibu wa UWT wilaya ya Ikungi, Yagi Kiaratu.
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, akitoka ndani ya ofisi ya CCM wilaya ya Ikungi baada ya kukabidhiwa fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa Singida.Nyuma ni mama yake, Mariamu Sepetu.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi
MSANII wa Filamu maarufu nchini Wema Isaac Abraham Sepetu,amechukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya viti maalimu CCM mkoa wa Singida na kuahidi kwamba lengo lake ni kuja kushirikiana na wanawake na wakazi kwa ujumla kuuletea maendeleo zaidi mkoa huo.
Wema ambaye amewahi kuwa miss Tanzania 2006,ameahidi kutumia nguvu zake zote na uzoefu wake katika kutumikia jamii,kusaidiana na wanawake katika kujiletea maendeleo yakiwemo na ya uchumi.
Alisema kwa muda mrefu amekuwa akiisaidia jamii ya jijini Dar-es-salaam na sasa ameamua kwa dhati kuelekeza nguvu zake katika kuitumikia jamii ya nyumbani kwao mkoa wa Singida.
“Pia natarajia kukaa chini na vijana wa mkoa wangu wa Singida,ili kwanza nijue chanagamoto zinazowakabili halafu kwa pamoja,tuweke mipango na mikakati ya namna ya kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo”, alisema.
Wema alisema kuwa ni nitaelekeza nguvu zangu kwa wanawake wenzangu…..nisikie vilio vyao ili iweze kupata mwelekeo wa namna ya kuwasaidia waweze kujiendeleza kwa manufaa ya familia zao,mkoa na taifa kwa ujumla.
Kuhusu sekta ya usanii,alisema endapo CCM kitampitisha na kufanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum,atatumia fursa ya kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kuwasaidia wasanii mbalimbali pamoja na mambo mengine,wasiibiwe kazi zao.
“Kwa kweli niwahakikishie wasanii wenzangu kuwa nikifanikiwa kuwa kiongozi,nitahakikisha kazi zao haziibiwi tena na pia kuwepo kwa mazingira rafiki yatakayo wasaidia kufanya kazi zao bila vikwazo vyo vyote”,alisema Wema.
No comments:
Post a Comment