Friday, 10 July 2015

SERIKALI YA UJERUMANI YATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUSIMAMIA NA KUENDELEZA MALIASILI.

1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru ( kulia) akiwa na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania, Dkt. Sussane Grimm ( kushoto) wakitia saini hati ya Makubaliano ya kusimamia na kuendeleza Maliasili nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Jijini Dares Salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House.


2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru ( kulia) akiwa na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania, Dkt. Sussane Grimm ( kushoto) wakibadilishana hati ya Makubaliano ya usimamizi na uendelezaji wa Maliasili nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Jijini Dares Salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House.
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz la nchini Tanzania imetia saini hati ya makubaliano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuendeleza na kusimamia Maliasili zilizopo nchini.
Hati hiyo ya Makubaliano imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhem Meru na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Giz nchini Tanzania, Dkt. Sussane Grimm .
Utiaji saini huo umefanyika Jijini Dares salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House, na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Bw. Herman Keryaro pamoja na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo 
Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania imeongeza kiasi cha Euro million tatu sawa na billion kumi kwa pesa za Kitanzania katika kusaidia usimamizi wa kiufundi ikiwemo uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Tanzania ( TAWA) . Pia Makubaliano hayo yatadumu kwa muda wa miaka mitatu katika kusimamia na kuendeleza Maliasili nchini.
Uhusiano kati ya Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ulianza mwaka 2014
Pia Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz nchini Tanzania imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii katika kipindi cha mpito cha Uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori ( TAWA) katika kuwandaa watumishi kufanya kazi katika Mamlaka hiyo .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!