Wednesday, 8 July 2015

Kutoka kikao cha maadili leo tarehe 08/7/2015..... Dodoma Kwalipuka

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Kanda ya Kaskazini, Kati na Ziwa wamesema iwapo Kamati Kuu (CC) na wale wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) watawaletea majina ya watia nia ambao ni wachafu, mafisadi na wenye kashfa mbalimbali watagoma kupiga kura.



Aidha, wamesema pamoja na mchakato huo kufuata taratibu na kanuni za chama wameitaka Nec na CC kuhakikisha majina ya Profesa Mark Mwandosya, January Makamba na Makongora Nyerere yanapita hadi hatua ya tano bora.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina wajumbe hao walisema wameajipanga vilivyo kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na mgombea mzuri ila hawatakuwa tayari kupiga kura kwa mgombea ambaye hana sifa.
Mmoja wa wajumbe hao ambaye anatoka Kanda ya Kaskazini alisema harakati zote za watu kununua urais zimeonekana wazi tangu mwanzo hivyo hawako tayari kuona nguvu hiyo ikitumika katika hatua yao.
Wamesema kutokana na uzalendo wao na hakuna msukumo wa mtu yoyote na iwapo hawatasikilizwa maoni yao Wanzania na CCM watarajie maamuzi magumu.

CHANZO: KENGETE BLOG

1 comment:

Bado habari haijatupa tunacho hitaji kufaham kuhusu mikutano hiyo Dodoma. said...

Bado habari haijatupa tunacho hitaji kufaham kuhusu mikutano hiyo Dodoma.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!