Monday 6 July 2015

KENYA YATANGAZA VITA VIKALI JUU YA MAPENZI YA JINSIA MOJA


Makamu wa Rais wa Kenya amesisitiza kuwa, serikali ya nchi hiyo haiwezi kuvumilia hata kidogo vitendo vya maingiliano ya watu wa jinsia moja. Msimamo huo wa William Ruto umekuja siku chache tu kabla ya kuwasilia Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya. 


Matamshi hayo ya Makamu wa Rais wa Kenya yamekuja kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo iliyodai kuwa watu wanaotenda vitendo hivyo vichafu wanayo haki kwa mujibu wa sheria za Kenya ya kuwa na chama chao. 

William Ruto amenukuliwa na vyombo vya habari akisema jijini Nairobi leo Jumapili kwamba, maingiliano ya watu wa jinsia moja ni kinyume na maumbile ya Mwenyezi Mungu. Amesema, Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanamme ili aolewe na mwanamme mwenzake wala mwanamke ili aolewe na mwanamke mwenzake. 

Amesema: "Tumesikia kuwa Marekani wanaruhusu ushoga na vitendo vingine vichafu. Ninapenda kusema nikiwa kiongozi Mkristo kwamba tutailinda nchi yetu ya Kenya na tutasimama imara kulinda imani yetu ya kidini na kulinda nchi yetu." 

Makamu wa Rais wa Kenya pia amewataka Waislamu na Wakristo kuunganisha nguvu zao na kusimama kidete kulinda imani zao mbele ya jaribio lolote la kutaka kuruhusu vyama vya mashoga nchini humo.

3 comments:

Anonymous said...


aziz bilal2:15 AM


1
Reply

Nasisi bongo tutatangaza lini vita na mambo ya ushoga,maana nasikia umekithiri sana siku hizi?.

Unknown said...

Dawa Yao ni kuweka sheria kali kwa wanaojihusisha na vitendo hivyo

Unknown said...

Dawa Yao ni serikali kuweka sheria kali kwa wanajihusisha na vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!