Friday 3 July 2015

ISIS NA UNYAMA ULIOKITHIRI


ISIS kwa mara nyingine tena wametoa video inayoonesha mambo ya kikatili wanayooendelea kuyafanya katika nchi za Kiarabu, ambayo inaonesha watuhumiwa wawili wa wizi wakimwagiwa kimiminka chekundu, ambacho kazi yake kubwa ni kuzuia kidonda kisipate maambukizi, kabla ya kukatwa miguu yao ya kushoto na mikono yao ya kulia kwa kutumia kisu kikali ambacho mara nyingi hutumika mabuchani kukatia nyama.

Wafuasi hao wa Islamic State ambao walishea video hiyo kwenye mitandao ya kijamii wanadai kuwa, wezi hao ambao walikuwa na silaha waliwashambulia wachungaji wa mifugo hiyo kabla ya kuiba mifugo na magari', mjini Homs huko Syria.
Hii imekuja siku chache tu baada ya mtu mwingine kuuawa baaada ya kurushwa kutoka juu ya Ghorofa mpaka chini kwa madai ya ushoga huko nchini Iraq.
 Moja ya watu wanaotuhumiwa kwa wizi wa mifugo akimwagiwa kimiminika chekundu na wanajeshi wa ISIS tayari kwa kukatwa mguu wake wa kushoto kwa kutumia kisu cha buchani.
Hapa kipande kilichokatwa kikifungwa bandeji haraka sana.
Wakijiandaa kumkata mkono
Tayari mkono umekatwa.
Akiwa kwenye ambulensi tayari kwa kupelekwa kusikojulikana.
Picha nyingine hii inaonesha wanajeshi wa ISIS wakiwarusha vijana wengine kutoka juu ya ghorofa mpaka chini kwa madai ya kushiriki ndoa ya jinsia moja.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!