Saturday, 4 July 2015

HAKIMU FEKI MBARONI KWA KUTAPELI SH. MILIONI NNE



Mkazi wa Kijiji cha Nyabisaga mkoani Mara, Jane Mahanga (24), aliyejifanya hakimu wa mahakama ya Mwanzo Sirari, amenaswa na kufikishwa katika mahakama ya Wilaya Tarime.'

 
Hakimu feki huyo amefunguliwa mashtaka matatu, likiwamo la kujifanya hakimu wa mahakama ya Mwanzo Sirari, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu kwa watu mbalimbali ikiwa pamoja na pesa taslimu Shilingi 4,000,000.
 
Mshtakiwa huyo ametupwa rumande hadi hadi Julai 16, mwaka huu, kwa mujibu wa mwenendo wa kesi yake inayoendelea katika Mahakama ya.Wilaya ya Tarime.
 
Alisomewa mashtaka hayo juzi katika kesi tatu za jinai iliyowasilishwa mbele ya Hakimu Dibogo Wenje. Mwendesha mashitaka wa polisi, Abel Kazen, alidai mtuhumiwa Jane Mahanga ambaye pia alijitambulisha kama Jane Dominick ama Jane Ryoba, mwaka uliopita aliwadanganya wafanyabiashara kadhaa akiwamo Simfroza Kibuti wa Tarime kuwa ni hakimu.
 
Alidai mtuhumiwa huyo alijifanya hakimu wa mahakama hiyo na kuchukua, mali kama nguo za dukani na fedha taslimu vyote vikiwa na thamani ya Shilioni milioni 2.5 kutoka kwa Kibuti akimwahidi kulipa lakini hakuonekana hadi alipokamatwa June 28, mwaka huu.
 
Kabla ya kutiwa mbarono alikuwa amewatapeli Lucas Ryoba wa Rebu Shilingi 300,000,pamoja na Shlingi  70,000 za vinywaji katika grosari ya Kantini ya Uhamiaji iliyoko Sirari.
 
Mshitakiwa huyo alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi wilayani hapo na walalamikaji wengi kujitokeza baada ya kudai kutapeliwa na mwanamke huyo.
 
Hata hivyo, alikana mashitaka yote yanayomkabili lakini aliwekwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini hadi Julai 16 mwaka huu, atakaposomewa tena  mashitaka 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!