Wednesday, 15 July 2015

AFYA YA MAMA MJAMZITO


Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke apate chakula bora. Ukosekanaji wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili. 


Kwa mama anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi yake vizuri na mwili kujitahidi kutoa protein kutoka sehemu nyingine za mwili kwa sababu hamna protein ya kutosha). 

Dalili zake ni pamoja na kuwa na protein kwenye mkojo, blood pressure kuwa juu, kuumwa kwa kichwa, kusikia kizungu zungu, kuzimia, kuvimba kwa viungo n.k


Mama mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.
Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora:

Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa: Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.

Mayai: Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protein, vitamins minerals na vitamin A ambayo itasaidia kuzuia infections.

Protein: Serving mbili ya samaki, maini , kuku, nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo au nguruwe, maharagwe au jibini. Kusaidia ujengaji mifupa, meno, misuli, ubongo na mwili kwa ujumla. Ukosekanaji wa protein ya kutosha kutasababisha kuchoka, uvimbe na kutojisikia kula au appetite ndogo.

Mboga za majani: Spinach, cabbage, collard greends, mchicha, matembele. Mboga hizi ziwe fresh na zile zenye rangi ya kijani iliyokolea(hizi ndio zenye virutubisho vya kutosha).  Mboga hizi zitakupa Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kuabsorb protein ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata anemia.

Whole Grains: Vipande vinne vya Mkate wa whole grain, mkate wa mahindi, vitaupa mwili vitamin B na carbohydrate kwa ukuaji wa misuli na nerves.

Vyakula vyenye vitamin C: Kipande kimoja au viwili vya machungwa au juisi ya ndimu, machungwa, nyanya. Vitamin C itasaidia uterus kuwa na nguvu ya kutosha ili kufanya kazi vizuri wakati wa labor, pia itasaidia kulinda mwili na infection na kusaidia kuabsorb iron kwenye mwili.

Siagi na mafuta: Serving tatu za maparachichi, siagi, olive oil au flax seed oil.

Matunda yenye rangi ya njano au orange: Huupa mwili vitamin A hii husaidia kulinda kibofu na figo kupata infections.

Maini kama unaypenda ni mazuri kwa protein pia.

Kunywa maji mengi ya kutosha. Maji huchangia kwa asilimia 75 ya uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji ya kutosha utaishiwa na nguvu kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya dehydration na kichwa kuuma.
`
Chumvi ya kutosha kusaidia kuzunguka kwa damu kutoka mwilini kwenda kwenye placenta. Kutopata chumvi ya kutosha kunaweza kusababisha miguu kuuma na uchovu.

Kwenye sehemu ya pili tutaongelea virutubisho kadhaa na umuhimu wake kwa mama mjamzito na mtoto.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!