Thursday, 18 June 2015

WABUNGE WAPONGEZA VILEO KUTOPANDA BEI

BAADHI ya wabunge wamepongeza hatua ya serikali kutoongeza kodi kwenye bidhaa za vileo, vinywaji baridi na sigara katika bajeti ya mwaka 2015/16 na kuwataka wazalishaji kutopandisha bidhaa zao.


Wakizungumza mjini hapa kwa nyakati tofauti, Mbunge wa Mtoni, Faki Haji Makame (CUF) alisema ni kunahitajika mipango madhubuti ya kuwadhibiti wafanyabiashara watakaokiuka au kukaidi na kupandisha kodi katika eneo hilo wakati serikali haijapandisha ushuru.
Alisema suala la kukuza uchumi wa nchi sio lazima kutegemea eneo hilo la vileo, vinywaji baridi na Sigara na kuwa kuna maeneo mengi ambayo serikali inaweza kuyatumia kama vyanzo vya mapato na kusaidia kukuza uchumi.
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (CCM), alisema serikali imefanya vizuri kuwa na chanzo kipya cha mapato.
Ngonyani alisema wafanyabiashara watakaoongeza bei kwa nguvu katika eneo hilo bila serikali kuongeza kodi watakuwa wamekiuka hivyo watastahili kuchukuliwa hatuakali za kiesheria ili iwe fundisho.
Mbungewa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema), alisema wafanyabiashara hawapaswi kupandisha bei katika bidhaa ambazo serikali haijapandisha kodi zake.
Alishauri serikali kuwa sikivu na kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwemo kodi za majengo, uvuvi na maeneo mengine kuliko kupandisha kodi katika maeneo ambayo matumizi yake ni ya lazima na kuwaumini wananchi wenye kipato cha chini.
Lyimo, pamoja na kuipongeza serikali kwa kuacha kutumia vileo kama chanzo kikuu cha mapato kila mwaka.
Kwa upande wake, Mbunge wa Mkinga, Dastan Kitandula(CCM), alitaka kupanda kwa bei ya mafuta kusitumike kama kigezo cha kupandisha bidhaa nyingine bei, na kuitaka Serikali idhibiti hali hiyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!