Sunday, 28 June 2015

USHAURI WA LEO: SABABU 14 KWANINI HUNA FURAHA

1. Una wasiwasi mwingi, kumbuka wasiwasi hautatui tatizo bali unaongeza.


2. Unapenda kuishi maisha ya kujilinganisha na wengine. Kila binadamu ni tofauti, ishi maisha yako, jipende kama ulivyo, jitume kwa malengo yako, usijilinganishe na yule, kila mtu ana shida zake.

3. Unang’ang’ania kuwa una uwezo wa ku control kila kila kitu. Hutaweza, mambo mengine yaache yaende.

4. Unataka kuwa mkamilifu, watu wakusema vizuri, kila kitu chako kiwe kamili. Hutaweza, hakuna mkamilifu chini ya jua.

5. Mtu wa visasi. Usiishi kwa visasi. Vinachoma na kukuchosha.

6. Unataka kila mtu awe kama unavyotaka. Kama uko fair basi unataka na wengine wawe fair kwako. Maisha hayaendi hivyo. Jiandae kwa lolote toka kwa binadamu, hawatabiriki.

7. Unadhani utakuwa na furaha endapo tu ndoto zako kwenye maisha zitafanikiwa. Hii itakutesa, sio kila ndoto lazima ifanikiwe. Kama uliota kujenga ghorofa, rizika kwanza unapoweza kuhama toka nyumba ya chumba kimoja kwenda yenye vyumba viwili. Maisha ni safari, na safari ni hatua. Furaha ya hatua moja inakujenga kifikra kuweza kuendea hatua ya pili.

8. Unatazama maisha kwa mtazamo wa glasi ya juisi iliyo nusu. Badala ya kuwaza mbona glasi iko nusu, furahia kwamba iko nusu na kunywa kilichopo, usisubiri ijae. Pengine haitajaa kamwe.
9. Una upweke, huna marafiki na wakati hilo linakutesa unawachunia hata wanafamilia na ndugu zako wa karibu. Familia ni kila kitu. Kaa nayo karibu, hata kama wanakukera namna gani. Sometimes familia sio lazima awe wa damu. Choose close people and make your own family.

10. Mtu wa kuwaza sana vitu katika maisha. Mara gari, mara nyumba, mara nguo, mara kiatu. Life is beyond materials. Love, laugh, just shukuru by being alive.

11. Una marafiki wasio na furaha. Kila siku wamenuna. Huzuni inaambukiza. Jitahidi uzungukwe na watu wenye furaha ya kweli. Furaha inaambukiza.

12. Bado hujagundua lengo lako kwenye maisha. Wewe mfanyakazi wa saluni, hela inaingia lakini unahisi unataka kufanya kazi benki, mara unataka kuimba, mara unataka kuwa mkulima Mbeya. Chagua moja, simama nalo.

13. Unakumbuka sana mambo ya zamani. Mara sijui msichana gani ulikuwaga naye miaka hiyo, mara sijui kampenzi gani. Potezea. Let the past be the past. Ishi sasa.

14. Hutaki kujifunza. Unadhani unajua kila kitu. Hata kama una miaka mingapi, kila siku jifunze mambo kadiri unavyoweza.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!