Friday 19 June 2015

Tuwe Wakweli: Tusimnange Wema Sepetu; Wengine Wanagombea Kwanini Asigombee? JAMII FORUMS



Yote Tisa: Kama watu wanaogombea wako hivi kwanini Wema naye asigombee? Ukikubali kina fulani wagombee basi na kina fulani nao waachwe wagombee. Watanzania wakiwachagua wataishi na uchaguzi huo kwa miaka mitano. Kama ana mashabiki wake katika Bongo Movie na hata nje ya Bongo movie kwanini asigombee? 




Nina uhakika kama ingekuwa ni Marehemu Kanumba watu wangeunga mkono tu - na alitangaza nia ya kugombea kwa wanaokumbuka.

Tusimnyanyapae kwa sababu ni mwanamke au ametumia vipaji vyake jinsi alivyotumia. Mbona Sugu aligombea akashinda na hajahukumiwa kwa Bongo Flava yake huko Mbeya bali kwa uwakilishi wake kwa wananchi wa Mbeya. Tumesikia Profesa J, Afande Sale wote wanania ya kugombea lakini sidhani kama wamehukumiwa kwa sababu ya muziki wao kwanini iwe kwa Wema?

Ilimradi anatimiza vigezo vya msingi - Rais wa Tanzania, Miaka 18 na hajawahi kufungwa kwa zaidi ya miezi sita (I think) basi aachwe agombee tu.

Lakini upande wa pili una ukweli pia; yeyote anayetangaza kugombea ajue pia ametoa haki ya wananchi kukosoa, kubeza na hata kutounga mkono kugombea kwake. Ndani raha ya demokrasia; siyo wote wanapaswa kumuunga mkono; haijalishi cheo gani. Ndio maana tupo wengine hatuwaungi mkono kina Lowassa na wengine.

Inawezekana tungependa agombee kwa chama kingine isipokuwa CCM; well, ndio uzuri mwingine wa demokrasia pia. Wengine wa Bongo Flava na Bongo Movie wamegombea nje ya CCM na ni haki yao; na wengine wenye kuamini CCM wagombee vinginevyo tutakuwa taifa lenye mawazo ya aina moja tu kama mashine. 

MMM

mwanakijiji@jamiiforums.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!