Wednesday, 24 June 2015

MTOTO WA BAKHRESA AJENGA AKARABATI MITAA ILIYO KARIBU NA JENGO LAKE LA KIFAHARAI

 KAWAIDA wanasiasa ndiyo wamekuwa watu wenye ahadi nyingi sana linapofika suala la maendeleo kwa jamii.

Mara nyingi wamekuwa wakieleza namna wanavyoweza kuwapatia manufaa wananchi kama watawachagua, mfano kuhakikisha wanapata maji safi, barabara bora na vinginevyo.


Wanasiasa wanajulikana kwa kutotekeleza ahadi zao na wengi wao wamekuwa wakishindwa kuzitekeleza kwa kutoonekana kabisa baada ya kupewa kura.

Halafu, wanaonekana kipindi kama hiki cha uchaguzi kwa kuwa kwa mara nyingine wanataka kupata kura, yaani wachaguliwe tena.

Kabla ya uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu, huenda wanasiasa wanaweza kujifunza kupitia Yusuf Said Bakhresa.

Yusuf ambaye ni mmoja wa wamiliki wa klabu ya Azam FC na Azam Media Group inayomiliki Azam TV, ameamua kumwaga takribani Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa barabara jijini Dar es Salaam.

Yusuf ambaye ni wakala wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), tayari ameishajenga mitaa miwili na anatarajia kujenga mingine miwili.


Mitaa yote ipo katika eneo la Msasani jijini Dar es Salaam, karibu kabisa na yalipokuwa makazi ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa barabara hizo umefanywa na wataalamu wa Kichina ambao badala ya kutumia lami kama ilivyozoeleka, Wachina hao wamejenga kwa kutumia saruji, wakitupia zege lenye unene mithili ya mikate mitatu iliyobebana!

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!