Asha - Rose Shaban Mtengeti Migiro ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na chama hicho tawala kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Migiro ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi, amewahi pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na sasa ni Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba.
Ndugu wanamzungumziaje?
Kaka wa Dk Migiro, Ally Shaban anasema dada yake huyo ni mtoto wa sita kuzaliwa katika familia ya mzee Shaban Mtengeti, yenye watoto kumi. Mtengeti alikuwa chifu wa Usangi, enzi za mkoloni hadi kwenye miaka ya 1960, Mwalimu Nyerere alipofuta uchifu.
Anasema tangu alipozaliwa, Dk Migiro amekuwa ni mtu wa watu asiyekuwa na makuu. “Anapenda watu na mtu asiyependa kuonewa,” anasema.
Kaka huyo anaendelea kueleza kuwa Dk Migiro ana nyota ya uongozi kwa kuwa ameanza kuongoza tangu alipokuwa chuo kikuu, ambako alikuwa mbunge kwenye Baraza la Vyuo.
Nafasi ya mwanamke katika uongozi
Ally anaeleza kuwa Dk Migiro ni mwanamke jasiri anayependa kusimamia haki na aliweza kuongoza Umoja wa Mataifa, hivyo anaweza pia kuongoza Tanzania.
Ally anasema uongozi wa mwanamke unasimamia sheria zaidi tofauti na uongozi wa mwanamume ambao wengi wameonekana wakipindisha sheria na kufichiana maovu kwa kigezo cha kulindana.
Wakazi wa Usangi wamzungumzia
Huwezi kuamini kwamba wakazi wengi wa Usangi hawamfahamu Dk Migiro kwa sura, huo ndio ukweli na baadhi wamesema hilo limetokana na daktari huyo wa falsafa za sheria kuishi muda mwingi jijini Dar es Salaam.
Migiro ameishi zaidi nje ya Mwanga kwa sababu mama yake ni mtu wa Dar es Salaam na kwa kiasi kikubwa amelelewa na mama na Mwanga alifika baada ya kifo cha baba yake.
“Migiro sijawahi kumwona, lakini nimekuwa nikisikia jina lake kwenye vyombo vya habari, hata huku anafika mara chache. Anakuja nyumbani, lakini kutokana na shughuli za hapa na pale sijawahi kufika kwake kumuona,” anasema Mohamed Kabewa mkazi wa Kijiji cha Mshewa Kata ya Chomvu.
Zaidi ya wakazi watano wa eneo hilo ambako ni nyumbani kwa Shaban Mtengeti, baba mzazi wa Dk Migiro, wameungana na Kabewa kueleza kuwa hawamfahamu Dk Migiro kwa kuwa haishi Usangi, badala yake maisha yote yako jijini Dar es Salaam.
Licha ya kutomfahamu Migiro, wananchi wa Kata ya Chomvu tarafa ya Usangi wanaamini kuwa anazo sifa za kuongoza kwa kuwa amewahi kuwa kiongozi katika maeneo mbalimbali na kote hakupata kashfa yoyote.
Anapoulizwa kwamba hadhani kama wakati wa mwanamke kuongoza nchi haujafika, Kabewa anasema: “Mfumodume kwa sasa hauna nafasi katika jamii na kwamba kwa sasa wananchi wanatakiwa kuangalia utendaji wa mtu na uwajibikaji wake katika jamii.”
Lakini kwa nyakati tofauti Hussein Mkodo na Rose Mfinanga wameonyesha mashaka kama mwanamke akipewa nafasi hiyo ya ngazi ya juu nchini ataweza kuongoza kutokana na hali ya nchi ilivyo.
Wakataja ufisadi na utawala bora kuwa ni matatizo makubwa yanayolikabili taifa sasa ambayo yanahitaji kiongozi makini kuyatatua.
“Siamini kama ataweza kukemea changamoto hizi kwani viongozi wengi wameonekana kushindwa, ila sio vibaya akijaribu,” anasema Mfinanga.
Kwa upande wake Mkodo anasema, wenye fedha wanaonekana kuvinunua vyombo vya dola kwa kuwa wana nguvu kuliko vyombo hivyo, hali anayosema kuwa hata Migiro akipewa nafasi ya uongozi wa juu itamuwia vigumu kupambana na wala rushwa.
“Utendaji wa Dk Migiro ni msafi kwa kuwa hatujasikia akituhumiwa popote, lakini tuna mashaka kama hao wanaosema milioni kumi ni hela za mboga ataweza kukabiliana nao kwa kuwa wako ndani ya chama,” anasema Mkodo.
Mkodo anasema kuwa kwa sasa Watanzania wanatakiwa kufanya mabadiliko kwa sababu kwa miaka 50 wamekunywa pombe ileile, lakini wanachokifanya ni kubadili chupa.
Anasema kwa sasa Watanzania wanaishi kwa mashaka, hawaioni hatma ya Serikali kwa kuwa viongozi waliopo wameshindwa kuisimamia na kusababisha wananchi kuishi maisha ya shida, huku wanasiasa wakijinufaisha kupitia migongo ya wanyonge.
Mfinanga anasema ufisadi wa nchi hii umeanza tangu enzi za Nyerere japo haukuwa umeshamiri kama sasa, lakini ufisadi ndio ulioviua vyama vya ushirika nchini.
“Tukisema tunamchagua mwanamke alete mabadiliko tunajidanganya kwa kuwa wote ni wa nyumba moja na hakuna anayeweza kusimama na kumshtaki mwingine, ….wataendelea kulindana na kufichiana uovu,” alisema Mfinanga.
Mkazi wa Usangi, Hashim Abdala anasema familia ya Dk Migiro ina kipaji cha uongozi kwa kuwa hata ndugu zake wana nyadhifa mbalimbali nchini. Lakini changamoto kubwa ni uovu unaofanywa na CCM na kuwafanya wananchi wakate tamaa.
“Mimi ni CCM tangu nizaliwe na sina mpango wa kukiacha chama changu, lakini viongozi wanakoipeleka nchi sasa ni kubaya na wananchi wamechoka na kukata tamaa,” anasema Abdala.
Mwanga. Asha - Rose Shaban Mtengeti Migiro ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na chama hicho tawala kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Migiro ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi, amewahi pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na sasa ni Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba.
Ndugu wanamzungumziaje?
Kaka wa Dk Migiro, Ally Shaban anasema dada yake huyo ni mtoto wa sita kuzaliwa katika familia ya mzee Shaban Mtengeti, yenye watoto kumi. Mtengeti alikuwa chifu wa Usangi, enzi za mkoloni hadi kwenye miaka ya 1960, Mwalimu Nyerere alipofuta uchifu.
Anasema tangu alipozaliwa, Dk Migiro amekuwa ni mtu wa watu asiyekuwa na makuu. “Anapenda watu na mtu asiyependa kuonewa,” anasema.
Kaka huyo anaendelea kueleza kuwa Dk Migiro ana nyota ya uongozi kwa kuwa ameanza kuongoza tangu alipokuwa chuo kikuu, ambako alikuwa mbunge kwenye Baraza la Vyuo.
Nafasi ya mwanamke katika uongozi
Ally anaeleza kuwa Dk Migiro ni mwanamke jasiri anayependa kusimamia haki na aliweza kuongoza Umoja wa Mataifa, hivyo anaweza pia kuongoza Tanzania.
Ally anasema uongozi wa mwanamke unasimamia sheria zaidi tofauti na uongozi wa mwanamume ambao wengi wameonekana wakipindisha sheria na kufichiana maovu kwa kigezo cha kulindana.
Wakazi wa Usangi wamzungumzia
Huwezi kuamini kwamba wakazi wengi wa Usangi hawamfahamu Dk Migiro kwa sura, huo ndio ukweli na baadhi wamesema hilo limetokana na daktari huyo wa falsafa za sheria kuishi muda mwingi jijini Dar es Salaam.
Migiro ameishi zaidi nje ya Mwanga kwa sababu mama yake ni mtu wa Dar es Salaam na kwa kiasi kikubwa amelelewa na mama na Mwanga alifika baada ya kifo cha baba yake.
“Migiro sijawahi kumwona, lakini nimekuwa nikisikia jina lake kwenye vyombo vya habari, hata huku anafika mara chache. Anakuja nyumbani, lakini kutokana na shughuli za hapa na pale sijawahi kufika kwake kumuona,” anasema Mohamed Kabewa mkazi wa Kijiji cha Mshewa Kata ya Chomvu.
Zaidi ya wakazi watano wa eneo hilo ambako ni nyumbani kwa Shaban Mtengeti, baba mzazi wa Dk Migiro, wameungana na Kabewa kueleza kuwa hawamfahamu Dk Migiro kwa kuwa haishi Usangi, badala yake maisha yote yako jijini Dar es Salaam.
Licha ya kutomfahamu Migiro, wananchi wa Kata ya Chomvu tarafa ya Usangi wanaamini kuwa anazo sifa za kuongoza kwa kuwa amewahi kuwa kiongozi katika maeneo mbalimbali na kote hakupata kashfa yoyote.
Anapoulizwa kwamba hadhani kama wakati wa mwanamke kuongoza nchi haujafika, Kabewa anasema: “Mfumodume kwa sasa hauna nafasi katika jamii na kwamba kwa sasa wananchi wanatakiwa kuangalia utendaji wa mtu na uwajibikaji wake katika jamii.”
Lakini kwa nyakati tofauti Hussein Mkodo na Rose Mfinanga wameonyesha mashaka kama mwanamke akipewa nafasi hiyo ya ngazi ya juu nchini ataweza kuongoza kutokana na hali ya nchi ilivyo.
Wakataja ufisadi na utawala bora kuwa ni matatizo makubwa yanayolikabili taifa sasa ambayo yanahitaji kiongozi makini kuyatatua.
“Siamini kama ataweza kukemea changamoto hizi kwani viongozi wengi wameonekana kushindwa, ila sio vibaya akijaribu,” anasema Mfinanga.
Kwa upande wake Mkodo anasema, wenye fedha wanaonekana kuvinunua vyombo vya dola kwa kuwa wana nguvu kuliko vyombo hivyo, hali anayosema kuwa hata Migiro akipewa nafasi ya uongozi wa juu itamuwia vigumu kupambana na wala rushwa.
“Utendaji wa Dk Migiro ni msafi kwa kuwa hatujasikia akituhumiwa popote, lakini tuna mashaka kama hao wanaosema milioni kumi ni hela za mboga ataweza kukabiliana nao kwa kuwa wako ndani ya chama,”
Mkodo anasema kuwa kwa sasa Watanzania wanatakiwa kufanya mabadiliko kwa sababu kwa miaka 50 wamekunywa pombe ileile, lakini wanachokifanya ni kubadili chupa.
Anasema kwa sasa Watanzania wanaishi kwa mashaka, hawaioni hatma ya Serikali kwa kuwa viongozi waliopo wameshindwa kuisimamia na kusababisha wananchi kuishi maisha ya shida, huku wanasiasa wakijinufaisha kupitia migongo ya wanyonge.
Mfinanga anasema ufisadi wa nchi hii umeanza tangu enzi za Nyerere japo haukuwa umeshamiri kama sasa, lakini ufisadi ndio ulioviua vyama vya ushirika nchini.
“Tukisema tunamchagua mwanamke alete mabadiliko tunajidanganya kwa kuwa wote ni wa nyumba moja na hakuna anayeweza kusimama na kumshtaki mwingine, ….wataendelea kulindana na kufichiana uovu,” alisema Mfinanga.
Mkazi wa Usangi, Hashim Abdala anasema familia ya Dk Migiro ina kipaji cha uongozi kwa kuwa hata ndugu zake wana nyadhifa mbalimbali nchini. Lakini changamoto kubwa ni uovu unaofanywa na CCM na kuwafanya wananchi wakate tamaa.
“Mimi ni CCM tangu nizaliwe na sina mpango wa kukiacha chama changu, lakini viongozi wanakoipeleka nchi sasa ni kubaya na wananchi wamechoka na kukata tamaa,” anasema Abdala.
Matarajio yao kwa Dk Migiro
Wakazi hao wanasema ikitokea CCM ikampitisha Dk Migiro wangetaka aanze kushughulika na mafisadi na ahakikishe amewachukulia hatua za kisheria ili arudishe imani ya wananchi iliyopotea.

MWANANCHI.

No comments:
Post a Comment