Mauaji ya kukata watu makoromeo yaendelea kutikisa Wilaya ya Bukoba, mpaka sasa watu 15 wameshauawa kwa kukatwa shingo kisha kukamuliwa damu.
-Usiku wa kuamkia jana, katika kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, wameuawa watu wawili huku wengine wakijeruhiwa.
Wilaya ya Bukoba (Manispaa ya Bukoba na Bukoba
Vijijini), Mkoani Kagera, kuna wimbi kubwa sana
la Mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.
Watu wasiojulikana LAKINI ambao bila shaka
wanafahamika kwa vyombo vya usalama, wanaua
watu.
Toka mwanzoni mwa mwaka huu, watu zaidi ya 15
wameuawa kwa kukatwa shingo na kuwakamua
damu.
Usiku wa kuamkia leo, katika kata ya Nyakato,
Bukoba Vijijini, wameuawa watu wawili huku
wengine wakijeruhiwa.
Wamekatwa shingo, wamekamuliwa damu
na kutupwa barabarani. Hivi ni kweli kwamba
Usalama wa nchi yetu umeshindwa kutambua
na kuwakamata wahusika wa matukio haya?
Wale waliokamatwa na kisha kuachiwa huru
nini kinaendelea?? Tunahitaji majibu.
Tunahitaji ulinzi na usalama wa wananchi
wenzetu wa Bukoba na nchi nzima.
Usalama wa Taifa, Polisi, Jeshi, tafadhali '
okoa maisha ya watanzania wanaouawa bila hatia.
No comments:
Post a Comment