Kim Kardashian akifanyiwa vipimo hospitalini jana, ambapo alionekana kuwa mjamzito. Aliyesimama kushoto ni mama yake, Kris Jenner.
MWANAMITINDO wa Marekani, Kim Kardashian, hivi sasa ni mjamzito akitegemea kumpatia mumewe, mwanamuziki, Kanye West, mtoto wa pili.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34, na ambaye mtoto wake wa kike aitwaye North atatimiza miaka miwili tarehe 15 mwezi huu, aliyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni Jumapili cha ‘Keeping Up With The Kardashians’.
Nyota huyo alimwambia dada yake Khole: “Nimepima damu hivi karibuni na nina ujauzito!” Wakati ndugu zake wakishangaa, mama yake, Kris Jenner, alisema anamsubiri mjukuu wake kwa hamu kubwa.
Kim alizaa mtoto wake wa kwanza Juni 15, 2013, na akafunga ndoa na Kanye Mei 24, 2014.
Kim alizaa mtoto wake wa kwanza Juni 15, 2013, na akafunga ndoa na Kanye Mei 24, 2014.
No comments:
Post a Comment