Wiki saba baada ya Liberia kutangazwa kuondokana na ugonjwa wa ebola, nchi hiyo imeripoti kuwepo mgonjwa mmoja wa ugonjwa huo.
Naibu waziri wa afya, Tolbert Nyenswah, amesema vipimo vimethibitisha kuwa mvulana wa miaka kumi na saba amekufa kutokana na ugonjwa wa ebola.
Amesema wataalam wanachunguza nyendo za marehemu kabla ya kifo chake.
Amewaonya wananchi wa Liberia kuwa kuwa waangalifu, lakini hakuna haja ya taharuki.
Kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa ebola katika nchi nyingine mbili za Afrika Magharibi zilizoathirika kwa ugonjwa huo Guinea na Sierra Leone, yakilipuka wakati mmoja na msimu wa mvua.
No comments:
Post a Comment