Thursday 18 June 2015

AZZY MLEMAVU MWENYE KIPAJI CHA HALI YA JUU



MSANII wa Hip Hop Bongo ambaye ni mlemavu wa viungo, Ahazi Eliah ‘Azzy’ juzikati alidhihirisha kipaji cha hali ya juu ‘alipotimba’ ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar leo.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya na Global TV Online, msanii huyo anayebamba kwa sasa na Ngoma yake ya Pole Mama aliyomshirikisha Sunday Mjeda ‘Linex’ aliongea mengi kuhusiana na maisha yake na kipaji chake.

“Uwezo wangu unajieleza, nina kiwango kikubwa cha kuchana lakini tatizo sijapata usimamizi wa kazi zangu. Sikuzaliwa mlemavu ni matatizo ya kupooza nilipofikisha miezi saba ndiyo yaliyonifanya niwe hivi,” alisema Azzy.
Kwa sasa Azzy hana msaada wa usimamizi wa kazi zake, ukitaka kumsaidia wasiliana naye kwa namba;
0716 751 795.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!