Saturday 20 June 2015

AJIRA JESHI LA UOKOAJI NA ZIMAMOTO NAFASI ZAIDI YA 1000

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
TANGAZO LA AJIRA

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania linatangaza nafasi za Ajira kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kwa vijana waliosomea ujuzi/fani, cheti na stashahada toka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wahitimu wa kidato cha sita na nne kati ya mwaka 2013 hadi 2014 waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Waombaji wa kazi watume barua za maombi kabla ya tarehe 30 Juni, 2015 kwa anuani ifuatayo:

Kamishna Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
S.L.P 5821,
DAR ES SALAAM.

1. SAJINI WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (SERGEANT OF FIRE AND RESCUE) – Nafasi 200.

Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha sita kati ya mwaka 2013 hadi 2014.
Mwenye Stashahada ya Habari na Mawasiliano, Utunzaji wa Kumbukumbu, Ugavi na Ununuzi, Katibu Muhtasi,Uhasibu na Uuguzi; au awe na cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la I katika moja ya fani ya Umakenika, Ufundi Bomba, Ufundi Umeme wa Majengo,Ufundi Umeme wa Magari, Wachora Ramani, Fundi Rangi wa Magari, Uchomeleaji, Ufundi Uashi, Gym, Ufundi Mitambo, Kada za Afyana Ufundi Seremala.

2. KONSTEBO WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (FIRE CONSTABLE) – Nafasi 803.

Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha nne kati ya mwaka 2013 hadi 2014. Mwenye cheti katika fani yaHabari na Mawasiliano, Utunzaji wa Kumbukumbu, Zimamoto na Uokoaji, Ugavi na Ununuzi, Katibu Muhtasi, Uhasibu na Uuguzi; au awe na cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la I katika moja ya fani ya Umakenika, Ufundi Bomba, Ufundi Umeme wa Majengo, Ufundi Umeme wa Magari, Wachora Ramani, Uchomeleaji, Ufundi Uashi, Gym, Ufundi Mitambo, Kada za Afya, na Ufundi Seremala. 
MASHARTI MUHIMU KWA MWOMBAJI: 

Mwombaji ni lazima awe amepitia na kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kati ya mwaka 2012 – 2015.
Waombaji wote wawe wamehitimu kidato cha sita na nne kati ya mwaka 2013 hadi 2014.
Mwombaji ambatanishe vivuli vya vyeti vyote yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari, cheti/vyeti vya taaluma na cheti cha kumaliza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), (CV) ikiwa na majina ya wadhamini watatu na anwani zao na picha mbili ndogoza (passpot size), hati ya kiapo haitakubaliwa.
Mwombaji aandike kazi aliyoomba juu ya bahasha.
SIFA ZA MWOMBAJI 

Mwombaji awe Raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25, mwenye afya njema na ambaye hajaoa au kuolewa.
Mwombaji asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
Mwombaji awe na urefu usiopungua sentimenta 155.
Mwombaji awe hajawahi kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.
Barua zote za maombi zitumwe kwa njia ya Posta.
Mwombaji awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote atakapopangiwa ndani ya Nchi.

Imetolewa na
Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji (T)
DAR ES SALAAM.

BONYEZA HAPA KU APPLY

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!