Tuesday 19 May 2015

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU MEI 2015/2016

 



ORODHA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJINGA NA MAFUNZO YA UALIMU 
AWAMU YA PILI MWAKA WA MASOMO 2014/2015



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) 
kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo 
ya Ufundi limechagua waombaji 2,543 (Me 1,651
 na Ke 892) kujiunga na Mafunzo ya Ualimu
 katika Awamu ya Pili ya Mwaka wa Masomo2014/2015. Waombaji 1,968 (Me 1226, Ke 742) wamechaguliwa
 kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa wanachuo
 (Central Admission System – CAS) na waombaji 575
 (Me 425,Ke 150) wamechaguliwa na Wizara ya Elimu
 na Mafunzo ya Ufundi. Majina ya waliochaguliwa
 yamewekwa kwenye tovuti ya NACTE
 (www.nacte.go.tz) na Wizara ya Elimu na Mafunzo 
ya Ufundi (www.moe.go.tz) na yametumwa
 kwa wakuu wote wa vyuo na maafisa
 elimu wa mikoa na wilaya.

Waombaji wamechaguliwa kujiunga na vyuo
 vya Ualimu vya Butimba, Tabora, Tukuyu
Mpwapwa, Kinampanda, Mhonda, Nachingwea, Singachini na Tandala. Vyuo vingine ni Tarime
 Bustani, Marangu, Morogoro, Klerru naSongea.
 Mafunzo ya Ualimu yataanza tarehe 01/06/2015 au la kama ilivyoelezwa kwenye fomu za maelekezo za chuo husika, hivyo wanachuo wanatakiwa kuanza kuripoti
 vyuoni kuanzia tarehe 28/05/2015. Fomu za
 Maelekezo ya Mafunzo (Joining Instructions) yameambatishwa. Pamoja na maelekezo yaliyopo
 kwenye fomu za kila chuo, mwanachuo anatakiwa 
kuripoti chuoni akiwa na vyeti halisi vya masomo 
na kwa ajili ya taratibu za usajili.

Mwombaji yeyote aliyechaguliwa ambaye chuo 
chake si miongoni mwa vyuo vilivyotajwa lakini 
ni chuo cha serikali ataweza kuomba uhamisho 
kwenye vyuo tajwa kwa kuandika barua au 
kupiga simu 0768 614045 la sivyo atajiunga
 na masomo mwezi Septemba 2015. 
Mwisho wa kupokea maombi ya uhamisho ni tarehe
 25 Mei 2015.


IMETOLEWA NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE 15/05/2015

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!