Mwanamke ambaye kakake alikufa katika ajali mbaya ya barabarani amekutana na mtu aliyepewa uso wake.
Amini usiamini mtu huyo aliyefanyiwa upasuaji huo wa kihistoria alipandikizwa uso mpya baada yake kuishi kwa miaka 15 akiwa bila pua.
Bwana huyo Richard Norris alimshukuru mwanamke huyo kwa niaba ya kakake marehemu aliyemwezesha kupata mwanzo mpya maishani.
Mwanamke huyo bi Rebekah Aversano alionekana akiugusa uso wa kakake akiwa haamini macho yake.
Bwana Richard Norris, anayetokea Virginia, Marekani alijeruhiwa katika ajali ya ufyatulianaji wa risasi miaka 15 iliyopita.
Yamkini Norris hakuwa amewahi kutoka nyumbani kwake katika kipindi hicho chote.
Kwa kawaida kwa sababu ya maadili ya utabibu watu waliopewa mabaki ya viungo vya wafu huwa hawakutani na jamaa za wale waliochangia, lakini Norris hakuweza kujizuia kukutana na bi
Aversano, kutoka Maryland.
Na alipomuona Bi Aversano, alibubujikwa na machozi na kusikika akisema ''hii ndiyo uso na sura niliyokuwa nayo''
Kakake Joshua Aversano, alipoteza maisha yake katika ajali mbaya ya barabarani akiwa na umri wa miaka 21.
kauli yake ya kutoa viungo vya mwili wake haikupokelewa vyema na familia yake na haswa mamake Gwen Aversano.
''Lakini kwa sababu hilo ndilo alilopenda sisi kama familia yake hatungempuuza'' alisema mamake katika mahojiano na runinga ya CTV.
''Baada ya kukutana na Norris aghalabu nimeweza kumuona mwanangu tena''
''Nahisi vyema kuwa nimemsaidia Norris kuanza upya maisha yake japo tumempoteza mpendwa wetu'' alisema mamake Joshua .
Upasuaji huo wa kihistoria ulifanywa katika chuo kikuu cha Maryland yapata miaka mitatu iliyopita.
Upasuaji ambao ulidumu kwa zaidi ya saa 36.
BBC
No comments:
Post a Comment