Saturday 2 May 2015

ALI KIBA AVAMIWA USIKU WA KUAMKIA LEO

Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba.
MSANII wa Bongo Fleva, Ali Kiba usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam, alivamiwa na kundi la watu wapatao 20 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.


Watu hao waliokuwa na silaha za aina tofauti yakiwemo mapanga, visu na silaha za moto walifanikiwa kuvunja kuingia ndani na kuwadhuru baadhi ya ndugu wa Ali Kiba na kuiba mali na kila kitu ambacho waliweza kubeba, walimpiga na kumtesa mlinzi wa nyumba hiyo wakimtaka awaonyeshe alipo Ali Kiba, hata hivyo hawakufanikiwa kumpata na wakaondoka muda mfupi kabla ya polisi hawajafika nyumbani kwa staa huyo baada ya kupigiwa simu na majirani.
Ikiwa utakuwa na taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa majambazi hao, unaweza kutoa taarifa katika kituo cha polisi ulicho karibu nacho.

IMG-20150502-WA0002
Reporter wa millardayo.com alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kupewa taarifa juu ya tukio hili, akafika Kunduchi Dar ambako Ali Kiba na mdogo wake Abdu Kiba wanaishi.
Nimeongea na Abdu Kiba, amesema yeye alikuwa Masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao.. waliovamia waliruka ukuta saa tisa usiku, wakavunja mlango wa sebuleni, wakakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, wakawapiga na kuwalazimisha wawaoneshe chumba ambacho Ali yumo.. wale vijana wakajibu kwamba Ali hayupo, wakaulizia chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu Kiba.
Wameingia chumbani wakamkosa Ali Kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia, pamoja na pesa milioni 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu.
Abdu amesema alitoa taarifa Polisi, wakafika usiku huo huo na kuanza ukaguzi wa eneo lote la nyumba.

Wakati tukio lote linaendelea Ali alikuwa ndani kwenye chumba kingine, hawakuomuona.
IMG-20150502-WA0000
IMG-20150502-WA0001
IMG-20150502-WA0002
IMG-20150502-WA0003
IMG-20150502-WA0004
IMG-20150502-WA0005
IMG-20150502-WA0006
IMG-20150502-WA0007
IMG-20150502-WA0009
IMG-20150502-WA0014
IMG-20150502-WA0018
Wale vijana wawili waliokutwa sebuleni wameumizwa kutokana na kupigwa, wametibiwa na kurudi nyumbani.. silaha walizoingia nazo hawajajua ila liko jiwe zito na chuma kizito ambacho kilitumiwa kuvunja milango wakati wanaingia.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!