Monday, 20 April 2015

WAWEKEZAJI WA KICHINA WANAVYOCHOMA MISHIKAKI TANZANIA

UWEKEZAJI wa Wachina nchini Tanzania umelalamikiwa na wananchi kwa watu hao  kufanya biashara za rejareja kama vile kuchoma mishikaki, kuuza nguo, simu na vitu vingine mitaani, jambo ambalo linawanyima fursa  wenyeji wasio na uwezo wa biashara kubwa.


Katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam si ajabu kukutana na baadhi ya Wachina wakiwa na biashara mikononi kama wafanyabishara wadogo nchini humo maarufu kama Machinga, hali inayozua mshangao na viulizo kwamba kweli hawa ni wawekezaji ama wamegeuka kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo!
Eneo la kibiashara la Kariakoo jijini Dar es Salaam ni mfano hai wa jinsi watu wa mataifa ya nje, zaidi ya Wachina, ambao wanafanya biashara za kawaida kama vile maduka madogo ya kawaida ambayo yanamilikiwa na Watanzania wa kawaida wenye mitaji midogo.
Swali ambalo Watanzania wanajiuliza ni kwamba wageni hawa ‘Machinga’ ni wawekezaji au ni watu waliokwepa macho ya serikali na kuingia mitaani kuwazibia riziki Watanzania!  Kama wanafanya hivyo kinyemela, ni nani hasa mwenye mamlaka ya kuweza kuwaondoa mitaani na kuhakikisha ‘uwekezaji’ wa aina hii unaondoka mitaani?
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!