Shirika la utafiti la Marekani limesema kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9 lilikumba eneo lililo umbali wa kilomita nane Mashariki mwa Pokhara Magharibi mwa mji Mkuu wa Kathmandu.
Kuna ripoti za uharibifu wa majengo na bidhaa, makazi ya watu hata miundo mbinu ya Mawasiliano ya simu nayo yameharibiwa vibaya.
Picha za majengo yaliyokuwa yameporomoka pamoja na mahekalu ya miaka mingi iliyopita zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii.
Walioshuhudia walisema kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.
Mitetemeko mingine midogo imesikika kaskazini mwa India pamoja na nchini Pakistan.
BBC.
No comments:
Post a Comment