Monday 27 April 2015

WARUNDI 152,572 WAHALALISHWA TANZANIA

Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile.
Waliokuwa wakimbizi wa Burundi zaidi ya 152,572 walioingia nchini mwaka 1972, wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania.

Wakimbizi hao walio omba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, sasa watakuwa raia halali wa Tanzania kwa kuwa na uwezo wa kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za udiwani na ubunge.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa vyeti hivyo jana, Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24, mwaka jana, katika Makazi ya Katumba mkoani Katavi, watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye kazi hiyo ilihamia katika Makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, ambako watu 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo.
Nisajile alisema katika makazi yake ya Mishamo ambako ugawaji wa vyeti hivyo unaendelea na unaotarajiwa kumalizika Aprili 30, mwaka huu, zaidi ya raia wapya 52,565 wanatarajiwa kupewa vyeti vyao.
“Mpaka leo (jana) katika makazi haya ya Mishamo kama unavyoshuhudia umati wa watu wanazidi kuingia, mpaka sasa tayari tumegawa vyeti 131,351 kwa raia hawa wapya na tunatarajia ifikapo Aprili 30 tutakuwa tumeimaliza hii kazi katika vijiji vyote,” alisema
Alisema Serikali inatoa vyeti hivyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR).
Hata hivyo, Nisajile alisema makazi ya Mishamo yana vijiji 16 na kabla ya kuanza kugawa vyeti, huwa wanatoa elimu ya uraia.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!