Monday, 20 April 2015

WAHAMIAJI 900 WAFARIKI DUNIA BAADA YA MASHUA YAO KUZAMA BAHARI YA MEDITERRANEAN

Maiti za wahamiaji waliozama baada ya mashua yao kupinduka nje ya pwani ya Libya siku ya Jumamosi zikiwa katika meli ya Italia katika bandari ya Malta.

Maiti zikitolewa katika meli hiyo.
Wahamiaji 28 wanaodaiwa kuokolewa wakiwa katika meli hiyo.
Meli ya Italian ikiwa katika harakati za kuwaokoa wahamiaji hao.
Wahamiaji hao baada ya mashua yao kuzama  wakiwa majini.
SIKU ya Jumamosi mamia ya wahamiaji wanaaminika kuzama baada ya mashua yao kupinduka nje ya pwani ya Libya.

Wahamiaji 900 wanadaiwa kufariki dunia wakiwemo watoto na wanawake, 28. Eneo ambapo mashua hiyo ilizama lina kina kirefu na huenda abiria wengi walikuwa wamekwama ndani ya mashua.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa njia kutoka kaskazini mwa Afrika kwenda Italia na Malta imekuwa eneo hatari zaidi duniani na makundi ya uokoaji yanastahili kuwa yanapiga doria eneo hilo.

Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, anasema kuwa mkutano wa dharura unahitajika kuandaliwa ili kuzungumzia suala hilo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!