Friday, 24 April 2015

Sitti Mtemvu kuzindua Taasisi, Kitabu na Kipindi chake cha TV May 2



 Taarifa ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, kwa vyombo vya habari leo imeeleza kuwa, Sitti atazindua kitabu kinachoelezea faida na hasara ya mitandao ya kijamii.



Amesema pamoja na kwamba mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri, huleta mapinduzi ya kimaendeleo ya kihabari kwa haraka.

Amesema maudhui yaliyopo katika kitabu hicho ni yanamlenga yeye moja kwa moja kama mhusika na kwamba pamoja na maumivu na athari azipatazo mhusika kitaelezea ni kwa jinsi gani ataweza kujifunza na kunyanyuka upya.

Mei 2, 2015 mwaka huu pia uzinduzi wa kitabu hicho utaenda sambamba na uzinduzi wa 'Taasisi ya Sitti Tanzania' yenye lengo la kusaidia watu wenye shida na kuweza kuendeleza gurudumu la maendeleo Tanzania.

Itakumbukwa sakata la Sitti kudaiwa kuwa ameghushi cheti cha kuzaliwa liliibuka kwenye kwa kasi mwaka jana kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyozifanya mamlaka husika kuanza kufuatilia uhalali wa cheti chake cha kuzaliwa....hadi pale alipojivua taji alilokuwa amevishwa baada ya kushinikizwa na watu mbalimbali kuwa aachie taji hilo kwa kile kilichoitwa ni kukosa uaminifu na kukosa sifa ya kushikilia nafasi hiyo.

=========



Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2014 na baadaye kulivua taji lake, Sitti Mtemvu, anatarajia kuzindua taasisi yake ya ‘Sitti Tanzania’, kitabu chake na kipindi cha TV kiitwacho ‘Chozi la Sitti.’


Uzinduzi huo utafanyika May 2 kwenye ukumbi wa Mlimani City na utapambwa na burudani kutoka kwa Yamoto Band.



No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!