skip to main |
skip to sidebar
RAIA WAANDAMANA KUSINI MWA CAROLINA NCHINI MAREKANI KUFUATIA DEREVA MWEUSI ALIYEPIGWA RISASI

WAKAZI wa jimbo la Kusini la Carolina nchini Marekani wameandamana kulaani mauaji ya dereva mweusi aliyepigwa risasi na kuuawa na polisi mzungu.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters, Waandamanaji hao ambao wengi wao walikuwa Wamarekani weusi wamesema kuwa yamefanyika kwa sababu za kibaguzi.
Katika mkanda wa video uliorekodiwa na shuhuda wa tukio hilo ulimuonesha polisi Michael Slager akimpiga risasi 8 za mgongoni dereva aliyetambulika kwa jina la Walter Scott.
Kesi ya Scott imezusha tena mjadala mkubwa nchini Marekani kuhusu mauaji yanayofanywa na polisi wazungu wa nchi hiyo dhidi ya raia weusi.
No comments:
Post a Comment