Thursday, 30 April 2015

MFUMO WA BEI WAENDELEA KUPAA

Mfumuko wa bei wa taifa kwa kipimo cha mwaka kwa mwezi uliopita, umeongezeka hadi asilimia 4.3 kutoka asilimia 4.2 mwaka huu.


 
Mfumuko huo ambao unapima kuwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi, umesababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula kama vile mchele, unga wa muhogo, nyama, samaki, maharage, choroko na sukari.
 
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia  mwezi uliopita, iliongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwapo kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kupaa kwa mfumuko huo ndani ya kipindi hicho kulienda sambamba na kuongezeka kwa fahirisi za bei kutoka 149.49 hadi 155.88 kati ya vipindi hivyo.
 
Kuhusu mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi nao umeongezeka kwa asilimia 0.7 kwa Machi ikilinganishwa na asilimia 1.6 kwa Februari mwaka huu ambao pia ulichangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma zikiwamo samaki, mchele, mbogamboga, machungwa ma sukari.
 
Pia, alisema,  uwezo wa Sh. 100 katika kununua bidhaa na huduma kati ya Setemba 2010 na Machi mwaka huu, umefikia Sh. 64 na Senti 15 kutoka Shilingi 64 na senti 59 kati ya vipindi hivyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!