Images credit: Reuters / AFP
Maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ya kugombea tena katika uchaguzi ujao wa Rais uliopangwa kufanyika nchini humo Juni mwaka huu yangali yanaendelea. Habari kutoka nchini humo zinasema kuwa, mbali na Bujumbura miji mingine kadhaa ya nchi hiyo imeendelea kushuhudia maandamano ya kulalamikia uamuzi huo wa Rais Nkurunziza. Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi limetangaza kuwa, idadi ya watu waliouawa katika machafuko yaliyoibuka nchini humo kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa muhula wa tatu yameongezeka. Alexis Manirakiza msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Burundi amesema kuwa, idadi ya waliouawa tangu kuzuka maandamano na malalamiko ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza ya kutaka kugombea kwa mara ya tatu katika uchaguzi ujao wa Rais uliopangwa kufanyika nchini humo Juni mwaka huu imeongezeka na kufikia watu sita. Alexis Manirakiza ameongeza kuwa, raia wengine saba wamejeruhiwa vibaya kutokana na vikosi vya usalama kuingilia maandamano hayo ya wananchi. Wakati huo huo, wanajeshi wa Burundi wametawanywa nchini humo kujaribu kukabiliana na wale wanaopinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza ya kutangaza kuwania muhula wa tatu. Wapinzani nchini Burundi wanaendelea kusisitiza kuwa, hatua ya Rais Nkurunziza.
No comments:
Post a Comment