Watuhumiwa wanne
wamekamatwa jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Bibi Titi na
Ohio karibu na Hotel ya Serena baada ya kumpora raia wa kigeni wakiwa na gari
dogo rangi ya kijivu yenye nambari za usajili T787 DBU Toyota Cienta.
Hivi karibuni kumeibuka
wimbi la wahalifu kuwapora pesa na vitu vya thamani kama mikufu, bangili, hereni
pia pete na vitu mbalimbali vya thamani raia wa kigeni na akina mama ambao
hupenda kutembea na pochi. Wahalifu hawa hutumia gari dogo ambalo mara kwa mara
hubadilishwa namba zake za usajili na wakati mwingine gari hili wanalitumia
kama Tax bubu.
Leo tarehe 21/04/2015
majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Posta Mpya watuhumiwa hawa
walimdangavya bwana CEES S/O JAN CONIJN, Miaka 27, raia wa Uholanzi aliyetaka
kufika Klabu ya Leaders kwamba wangempeleka eneo hilo kwa kutumia gari tajwa
hapo juu. Baada ya kuondoka na dereva kila baada ya mita 200 dereva huyo
alikuwa anasimamisha gari na kuongeza mtu mwingine kama abiria hadi walipotimia
wote wane.
Walimpeleka hadi maeneo
ya Kinondoni kwa Manyanya na walipofika eneo hilo walimweleza wazi kuwa wao ni
wahalifu na walimtaka awapatie pesa vinginevyo wangemuua. Aliwapatia pesa zote
alizokuwa nazo Tshs 75,000/= lakini hawakuridhika ndipo walipomtaka awapatie
kadi ya benki (ATM CARD) na nambari za siri (Pass Word).
Baada ya tukio hilo
wakamtupa karibu na Hospitali ya Mwananyamala na wao wakageuza gari kurudi
katikati ya mji. Wakati tukio hilo
linatokea raia wema walishuhudia na kutoa taarifa kwa Polisi. Polisi
walifuatilia haraka na kuweka mtego uliowanasa watuhumiwa wote katika eneo la
makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena.
Majina ya watuhumiwa
waliokamatwa ni:
1.
SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25,
Mkazi wa Chang’ombe Bora.
2.
ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka
30, Mkazi wa Kimara Temboni.
3.
MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka
27, Mkazi wa Mwananyamala.
4.
STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING,
Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.
Walipopekuliwa
watuhumiwa hawa walikutwa na simu
mbalimbali za mkononi zipatazo 11 ambazo zinachunguzwa kuhusiana na
mbinu ya uhalifu wanaoutumia. Pia ilikamatwa ATM CARD iliyochukuliwa kwa
mlalamikaji kabla watuhumiwa hao hawajaitumia. Aidha gari namba T787 DBU Toyota
Cienta linashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Miongoni mwa watuhumiwa
waliokamatwa, wawili ambao ni MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, na STEPHANO S/O
ALBERT KIKINDI @ KING, tayari wanazo kesi nyingine mahakamani na wako nje kwa
dhamana.
Sambamba na tukio hili
oparesheni ya kuwakamata wahalifu wengine wenye mtindo huu wa kuwapora wageni
au wakina mama wenye mikoba inaendelea na tunawaomba wananchi waonyeshe
ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza vitendo hivyo viovu. Aidha hakuna silaha
yoyote iliyotumika au kukamatwa kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali
ya kijamii.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.<
DAR ES SALAAM.<
No comments:
Post a Comment