Sunday, 26 April 2015

LEO NI MIAKA 51 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

RAIS Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, leo atawaongoza watanzania katika kuadhimisha miaka 51 ya kuzaliwa kwa Tanzania baada ya kuunganisha nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.

Muungano huu umeasisiwa na mashujaa wa nchi hii ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume tarehe 26/4/1964.
Muungano huo ulifanyika baada ya nchi hizi mbili kujipatia uhuru wake ambapo Tanganyika ilipata uhuru mwaka Desemba 1961 na Zanzibar Januari 1964.
Katika sherehe hizi watanzania watashuhudia matukio kadhaa yakiwemo ya kijeshi ambapo gwaride lililioandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama litapita kwa mwendo wa taratibu na mwendo wa kasi pamoja na ndege za kivika kupita huku zikionesha manjonjo yake katika kutoa heshima kwa Amiri jeshi Mkuu.
Mbali na hayo pia kutakuwa na halaiki ya watoto wakionesha mambo mbalimbali yanayohusiana na sherehe hii ya leo. Ndani ya miaka hiyo 51 mataifa hayo yamepiga hatua katika maendeleo makubwa tofauti na wakati zinaungana.
Maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja, Ipigie Kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!