Monday, 20 April 2015

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LINAENDELEA KUFANYA UCHUNGUZI KWA WATU WANAOHUSIKA NA KUENDESHA VITUO VYA KULELEA WATOTO AMBAVYO HAVIJASAJILIWA KISHERIA



Kamamti ya ulinzi na usalama ya Wilaya ikiwasikiliza mmoja wa watoto hao.



Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kufanya uchunguzi wa watu wanaohusika na kuendesha vituo vya kulelea watoto ambavyo havijasajiliwa na vinaendeshwa katika maeneo ambayo ni hatarishi kwa watoto.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya wakiangalia sehemu ya jikoni walipokuwa wakipika.
Kamanda MISIIME amesema Polisi iligundua vituo vitatu katika eneo la Nkuhungu Dodoma Mjini baada ya kupokea taarifa kwamba kuna nyumba ambazo zinaonekana kuingia watoto wengi na inawezekana siyo mazingira salama ya kuishi binadamu hasa watoto na wanachofundishwa huenda ni kinyume cha maadili.




Moja ya chumba cha kulala kikiwa na mizigo mbalimbali
Ameendelea kusema kuwa majira ya saa sita na nusu usiku (00:30) tarehe 17.04.2015 Polisi walipofika katika eneo la kwanza walikuta watoto 63 kati yao 46 wana umri chini ya niaka 18 ambapo wadogo kabisa wana umri wa miaka 6. Kituo cha pili wamekutwa watoto 40 ambapo kati yao walio na umri chini ya miaka 18 ni 12.
Chumba cha kulala kikiwa na vitu mbalimbali
Pia Kamanda MISIME amesema kituo cha tatu wamekutwa watoto 7 na wenye umri wa chini ya miaka 18 ni 5, hivyo kufanya watoto walio chini ya umri wa miaka 18 waliokutwa katika vituo hivyo vitatu ni 63 na wenye umri wa miaka 18-25 ni 52.
Darasa ambalo pia hutumiaka kama chumba cha kulala pamoja na kuswali.
Watoto wote hao ni wa kiume na wengi wanatoka Wilaya ya Kondoa  watoto 50, Dodoma Mjini, Chamwino na Mpwapwa jumla wako watoto 26 na waliosalia wanatokea Mikoa ya Kagera, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Zanzibar, Tanga, Tabora, Singida, Pwani, Lindi, Mtwara, Geita, Mwanza na Manyara. Watoto hao wamekutwa wamechanganywa bila kujali umri katika mazingira ambayo kiuhalisia ni hatarishi.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya Betty Mkwasa akiongea na watoto hao.
Uchunguzi unaendelea na yeyote atakayeguswa na ushahidi kuwa amekiuka sheria atafikishwa mahakamani ikiwepo wazazi walioruhusu watoto hao kuwa katika uangalizi ambao siyo wa kutosha kama sheria ya watoto ya mwaka 2009 inavyoelekeza.
Vile vile Kamanda MISIME amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kuchunguza walikuwa wakifundishwa kitu gani na kama walikuwa wakihudhuria Shule kulingana na umri wao na sheria za nchi zinavyoelekeza.

Chakula kilichobaki na kuhifadhiwa sehemu ambayo si salama.
Ametoa wito kwa familia, Viongozi wa Serikali za mitaa, dini na taasisi nyingine kutoruhusu watoto wao kupelekwa na kulelewa katika vituo hatarishi.
Aidha amesema watakapoona katika maeneo yao, himaya zao vituo kama hivyo visivyosajiliwa na hatarishi kwa watoto watoe taarifa mapema. Aidha wasiruhusu au kufumbia macho vitendo vyote vya kiuhalifu kuendeshwa katika maeneo yao kwani wakigundulika hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria.
Nyumba iliyokuwa inatumika kama shule na nyumba ya kulala.
Sehemu ambayo inatumika kama tenki la kuhifadhia maji kwa shughuli mbalimbali.
Chumba cha kulala kikiwa na vitu mbalimbali
Pia Kamanda MISIME amesema wazazi wanaofahamu kwamba watoto hao ni watoto wao wajitokeze ili kupewa maelekezo wasisubiri kutafutwa.

KWA HISANI YA PAMOJA BLOG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!