Mwili wa Marehemu Mbita ukiingizwa kwenye gari maalum la Jeshi kwa ajili ya kupelekwa makaburi ya Kisutu Dar kwa maziko.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akiwa katika jukwaa lililokuwa limeandaliwa katika Makaburi ya Kisutu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa nne kushoto) akiwa katika jukwaa lililoandaliwa katika makaburi ya Kisutu.
Brasbendi ya JWTZ ikiongoza maandamano ya waombolezaji katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Majenerari wastaafu (kushoto) wakiongozwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba aliyevaa kombati wa tatu kulia.
Wanajeshi wa JWTZ wakiwa kwenye paredi maalum la mazishi ya Brigedi Mbita katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akitoka kuweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Brigedia Mbita kama inavyoonekana pichani.
HATIMAYE mamia ya wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana walijitokeza kumzika aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika, Brigedia Jenereli Mstaafu Hashim Mbita.
Kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mwili wa marehemu Mbita ulifikishwa katika msikiti wa Kwa Mtoro Kariakoo kwa swala maalum ya mazishi.
Marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita alizaliwa Novemba 2, 1933 katika kijiji cha Songoro, mkoani Tabora. Katika utumishi wake alishika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Ofisa Habari Mkuu wa Serikali mwaka 1962 hadi 1965 na mwandishi wa habari wa rais 1965 hadi 1967.
Marehemu Mbita pia enzi za uhai wake aliwahi kuwa Mwalimu wa siasa katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli mwaka 1969 hadi 1970, Katibu wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, 1972 hadi 1989 na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe kuanzia 2003 hadi 2006.
Brigedia Jenerali Hashim Mbita alifariki dunia Aprili 26 mwaka huu katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo na alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment