Wednesday, 29 April 2015

BAADA YA KUTANGAZWA KUWA MAREHEMU KAZIKWA NA VITU VYA THAMANI, WEZI WAFUKUA KABURI

KaburiImetokea Kibaha kwenye mkoa wa Pwani Tanzania, ilitangazwa kwamba Marehemu kazikwa na vitu vya thamani ambavyo akiwa hai alisema angependa azikwe navyo, maziko yakafanyika salama akazikwa na sanduku lake.


Baada tu ya kuzikwa kuna mlinzi alipewa kazi ya kulinda kaburi mpaka likauke ambapo baada ya kulinda kwa zile siku walizokubaliana, siku ya kwanza baada ya siku za mlinzi kumalizika Wezi wakaja kulifukua kaburi kama inavyoonekana hapo juu na wakaiba sanduku, wakamvua Marehemu soksi na inasemekana walitaka kumvua na nguo zake pia ikashindikana.
AW1A3741Hizi ni picha ambazo nimekusogezea hapa.. ndugu waliamua kulijenga upya baada ya wezi hao kubomoa na kuiba vilivyokuwemo ndani.
AW1A3731Shuhuda anasema hata hivyo baada ya kaburi kubomolewa na wezi, mtu mmoja ambaye alikua akikata majani maeneo ya karibu na makaburi alisema ameona nguo zilizotawanywa kutoka kwenye sanduku na ikajulikana ndizo alizozikwa nazo Marehemu, zikakusanywa na kuchomwa moto.
AW1A3735
AW1A3736
AW1A3738
AW1A3741Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha tukio hilo, linawatafuta waliovunja kaburi hilo na kufanya uhalifu wa kuiba nguo na vitu vingine alivyozikwa navyo.
vlcsnap-2015-04-28-17h50m41s139
vlcsnap-2015-04-28-17h49m47s112
Shuhuda wa tukio hilo
Chanzo: Millard Ayo.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!