Wednesday 25 March 2015

Watoto 13,000 nchini huzaliwa na magonjwa ya Moyo

DOKTA NAMALA

Imeelezwa kuwa, zaidi  ya watoto 13,000 nchini, wanazaliwa na magonjwa ya moyo huku kati yao asilimia 25 pekee, wanahitaji matibabu ya ndani kwa kipindi cha mwaka mmoja mara baada ya kugundulika.


Aidha, mwaka 2013/14 jumla ya watoto 330 walihitaji matibabu, kati yao 128  walifanyiwa upasuaji.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam, na Makamu wa Rais wa Chama cha Madakatari wa Watoto Tanzania, Dk. Namala Mkopi(pichani), mbele ya waandishi wa habari.
Pia, chama hicho kwa kushirikiana na asasi ya ‘Save a Child Heart’, kutoka nchini Israel, na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wameratibu mpango wa kuwatambua watoto wenye ugonjwa wa moyo na kuhitaji vipimo vya awali, tiba pamoja na upasuaji.
Alisema kuwa, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kuanzisha kitengo maalum cha kutoa huduma za kisasa, vipimo ambavyo vinaweza kugundua magonjwa ya moyo kwa watoto.
“Pamoja na kitengo hiki kufanya baadhi ya matibabu bado hakijaweza kufanya upasuaji hususanI kwa watoto kutokana na hilo wizara ya afya inajitahidi kuwapeleka watoto hawa nchini India kwa ajili ya upasuaji,” alisema Dk. Mkopi.
Pia alisema chama hicho kimeingia makubaliano na asasi hiyo, ili kuwasafirisha nchini Israel, watoto wenye ugonjwa wa moyo kupatiwa matibabu, vilevile watagharamiwa huduma zote.
Na Modewji blog team

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!