Halo Mwanangu Chriss, Ni miaka minne sasa Tangu ulipoondoka nyumbani kwa lengo la kutafuta Maisha huko ulipoenda. Najua kazi zitakua zimekuzidi mpaka kupelekea Ushindwe hata kutujulia hali. Nilipatwa na wasiwasi niliposikia kuwa kuna Mabomu yalilipuka na kuua watu huko Mjini ulipokuwepo.
Nikajua ukimya wako pengine na wewe ulikumbwa na dhoruba hilo. Mwanangu Baba yako alikufa kwa Presha baada ya Shamba lake kuuzwa baada ya kushindwa kulipa ile pesa ya nauli aliyekopa kwa mjumbw ili uweze kusafiri kwenda huko dar. Nilijawa na Matumaini nilipoambiwa na RITAH kuwa siku mbili kabla ya kuja huku alikuona uwanja wa ndege wa DUBAI ukielekea America kwa Matembezi... Hofu yangu sikujua je ni kwanini hukumpa salamu aniletee. Ila nikaona si hofu labda RITAH hukumkumbuka sasa ila Mbona yeye alikujua..?
Majuma na miezi yakatika Mbona Sikuoni, Na hofu ya kupoteza sura yako naona inakaribia. Nguvu ya macho uliyoniacha nayo si ile tena, sasa siwezi kuona vya Mbali, Hata miguu yangu sasa imekwisha nguvu... Sura yangu imepoteza Tabasamu.
Zile safari za shambani kila siku asubuhi zimemaliza mifupa yangu.
Chriss Nasikia sasa umenipatia Mjukuu aliyechanganya Rangi... Ningependa kumuona pengine Amefanana na babu yake.
Nini kimekukumba CHRISS wangu...? Nilijisikia furaha zaidi niliposikia unaonekana kwenye Tv kuwa ni bingwa wa Kugawa pesa katika matamasha ya wanamuziki...
Nakuomba uipatapo Barua hii kumbuka pia kuna MAMA yako huku kijijini.
Njoo kwenye Kaburi langu uniage pengine ukichelewa kupata barua hii... Sidhani kama nitapona kwa kuwa lile figo moja nililobakiwa nalo baada ya kukuwekea wewe Moja.. hili nililobakiwa nalo halifanyi kazi tena.
NAKUPENDA SANA MWANANGU.
Wako MAMA.
Imetumwa October Mwaka juzi
Imepokelewa March 2015
No comments:
Post a Comment