Sunday, 29 March 2015

MATAIFA YA KIARABU KUBUNI JESHI LA PAMOJA

Rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi


Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi amesema kuwa viongozi wenzake wa nchi za kiarabu wamekubali kuunda jeshi la pamoja.
Bwana al-Sisi alipendekeza hili kukabilina na kile alicho kitaja kuwa tisho linalokabili eneo hilo.
Makubaliano hayo yaliafikiwa wakati wa mkutano wa nchi za kiarabu ambao umetawaliwa na mzozo ulio nchini Yemen.
Kikosi cha pamoja kinachoongozwa na Saudi Arabia tayari kiko eneo hilo kikiwalenga waasi wa kishia wa Houthi.
Muungano huo unasema kuwa kampeni dhidi ya waasi wa houthi zitaendelea hadi wakati watakapoweka silaha chini na kuondoka maeneo waliyoyateka

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!