Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kuanza ziara ya siku mbili wilayani humo tarehe 13.3.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mwalimu Mariam Halfan Haji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kama ishara ya upendo na kumkaribisha rasmi kutembelea wilaya ya Mafia.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau alikuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliofika kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ajili ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili wilayani humo tarehe 13.3.2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Akina mama wa Mafia waliofika kumpokea Mama Salma Kikwete wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia wanaonekana wakiwa wamebeba mabango ya kumkarisha wilayani humo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi/albino aliyekuwa amebebwa na mama yake. Mama Salma alikutana na mtoto huyo wakati alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau akitoa maelezo mafupi kuhusu Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia ambayo imejengwa na “Mafia Island Development Foundation, MIDEF”. Dkt. Dau ni mmoja wa viongozi wa Taasisi hiyo. Mama Salma alitembelea Shule hiyo tarehe 13.3.2015. Waliokaa kutoka kushoto ni Mbunge wa Mafia Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo, Ndugu Mohamed Msosa, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo na mwisho ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mafia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi.
PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment