Friday 13 February 2015

VALENTINE NI NINI?

Leo nimeona niongelee kidogo nini maana ya Valentine kwa asili yake kisha kila mtu kwa Imani yake na mapana yake akatambua kuwa anapokuwa sehemu ya Valentine Day anakuwa ana adhimisha nini na kwa sababu gani wengi tunasheherekea kama sio kuadhimisha Valetine Pasipo kujua asili yake.

Valentine’s Day kama Sikukuu Ya Kipagani:
Valentine’s Day si siku ya Sikuu ya Kikristo, hata kama jina lake asili yake inatokana na Ukristo  haiwezi kuhalalisha sasa Valentine kuwa Siku Ya Kikristo. Tukiangalia suala sikukuu hii kwa jicho la tatu, hatuoni uhusiano mkubwa kati ya watu wa Mungu  na Malove dove yaani mapenzi. Kuna mambo mengi yanaweza ibua mjadala na kutokuelewana miongoni mwa jamii ya wakristo na wasomi juu ya chimbuko ya Siku ya wapendanao al maarufu Valentine’s Day. Hatutaweza kamwe kuwa na uwezo wa kuwa na jibu muafaka kuhusu uhalali wa kusheherekea valentine kwa namna moja ama nyingine kutokana na tofauti za  kitamaduni na kidini ili mwisho wa siku tujenga upya hadithi kamili na madhubuti, lakini uhusiano kipagani hadi sasa na nguvu zaidi kuliko wale wa Kikristo kwa namna yoyote ile.

Februari 14 & Juno Fructifier au Juno Februata (
February 14th & Juno Fructifier or Juno Februata)
Enzi hizo Warumi walikuwa wakisheherekea  kwa kupumzika kabisa kama sikukuu ya muungano ama sikukuu zozote za hapa bongo kila  Februari 14  kama siku ya kutoa heshima kwa Juno Fructifier. Huyu Juno Fructifier alikuwa nani?huyu alikuwa  Malkia wa miungu ya Kirumi ambaye alikuwa Mungu mke kama mmoja wapo wa  miungu ya ndoa kama ndo zilikuwa zinasua sua basi tarehe 14 February ndo ilikuwa kama siku ya kufanya matambiko. Enzi hizoilikuwa  Katika sherehe moja, wanawake walikuwa wakiwasilisha majina yao na kuweka kwenye kisanduku na baadae wanaume wangepita mbele ya kisanduku hicho na kila mmoja kujitwalia jina moja. Kilichokuwa kinatokea katika sherehe kila aliyejiokotea jina hulitaja na kujitwalia huyo mwanamke kuwa mwanandoa kwa muda wote wa sikukuu wakati mwingine ilikuwa ni mwanandoa wako kwa mwaka mzima mpaka Valentine nyingine akaweke jina pale kwenye kibox. Mila hii ilitumika kukuza Jamii ya Kirumi kwa maana ya uzazi na maisha mengine kwa ujumla, kasheshe kama ulibeba ile ya mwaka mzima then Valentine imefika kisha unataka kubadilisha halafu uliyembeba mwaka jana mjamzito tehe tehe imekula kwako.

St Valentine,  Padri Wa Kikristo (
St. Valentine, Christian Priest)
Kulingana na hadithi za zamani, Mfalme wa Kirumi mwenye jina Claudius II ilipiga marufuku juu ya ndoa kwa sababu enzi hizo vijana wengi walikuwa wakiojitwalia wake mapema ili kukimbia jeshi maana amri ilikuwa mtu ambaye hana mke hana familia ndo alikuwa anapaswa kuingia jeshini maana hana cha kupoteza yuko mwenyewe tuy tehe tehe. Sasa kuna Padri mmoja wa Kikristo aitwaye Valentinus yeye ndo alikuwa kazi yake kufungisha hizo harusi kisirisiri maana inaonekana walikiuwa wakimpoza na mwisho wa siku huyu padri akahukumiwa kunyongwa. Wakati akisubiri kunyongwa, Wapenzi Vijana (Couples) walimtembelea  na kumwandikia kitu kama barua kama sio waraka kuwa ni namna gani ndo ni tamu kuliko Vita ya kwanza vya dunia na vya pili.
Valentine Mwingine.
Valentinus mwingine alikuwa Padri nae alifungwa  jela kwa ajili ya kusaidia Wakristo. Wakati akiwa bado yuko jela huyu kuhani aka fall in love na binti mlinzi wa gereza na wakati karibu anakwenda kunyongwa akaandika ujumbe “From Your Valentine” . Habari zake zikahifadhiwa na kuripotiwa Papa Julius I na baadae alijenga nakshi nakshi  juu ya kaburi lake.

Wakristo Wajibinafsishia Valentine’s Day:

Katika  mwaka wa 469 wa kutawala kwake Gelasius alitangaza Februari 14 siku takatifu kwa heshima ya Valentinus tajwa hapo juu badala ya kuwa siku ya kipagani ya mungu Lupercus wa Kirumi. Hapa ndo Wakristo wa enzi hizo wakachakachua sikukuu hiyo na kuruhusu kuchukua baadhi ya maadhimisho ya siku ya mapendo na ngono ambapo awali mambo hayo yalikuwa katika mazingira ya upagani. Si ajabu kwenye Valentine hii ukaona Guest House zimejaa, madukani watu wananunua condom hawajui kuwa kuadhimisha huko hawajaanza wao ila ni zile imani za kipagani. Maadhimisho ya kipagani yalikuwa lazima yaitimishwe kwa tendo la ngono ili kuonesha kilele cha upendo. Na njia rahisi iliyokuwa ikitumika katika kusheherekea siku hii ni ile ya kuweka majina kwenye kibox kisha kilaini unajibebea huku “mungu” Shahidi akisimamia zoezi zima. Kwa maana ya kwamba hakuna mtu atakaye okota jina bahati mbaya kuna roho inayomuongoza mtu kuchagua jina fulani.

Valentine Day Yageuka kuwa Siku Ya Wapendanao.
Kama ambavyo tumeitazama siku ya Valentine wala haikuwa siku ya wapendanao ilikuwa sikukuu ya Kipagani, ila baadae ikachakachuliwa hapo ikawa ya Kikristo lakini ni kama upagani ndani yake. Ilipokuwa Wakati wa Uamsho kwente Karne ya 14 ambapo tamaduni zikaanza kupewa tena shamrashamra za Kitaifa, ndipo Valentine ikapewa shavu la kuwa siku ya wapendanao. Ndipo katika kipindi hiki watu wakaachana na makatazo ya kidini wakati huo na yale mafundisho ya msingi katika dini yakapewa kisogo na watu wakageukia matamanio yao.Nyaraka na nyimbo mbali mbali za kuhusu mapenzi, ngono na kujamiiana vikaenea katika kizazi hicho kama ilivyo sasa kila nyimbo ni mapenzi hata picha za mabango ya barabarani ni mapenzi kwenda mbele.

Valentine na Kibiashara  Zaidi.
We utaona tu valentine hii ubepari unavyoshika hatamu yake katika kutumia ili tu “Wapenzi” Wakolezee eti Valentine Day. Kuna watu watanunua nguo mpya nyekundu ili mradi tu watupie kitu chekundu, mijihela mingine itapelekwa kununulia zawadi za wapenzi, hapo sijahesabu maua yatakayonunuliwa siku ya valentine, hapo sijaongelea chakula cha usiku cha wapenzi, hapo sijaongelea wale watakao amua kwenda kulala. Kama kuna siku nzuri ya biashara basi Valentine inakaribiana na Christimas.
Mtazamo Wangu na Valentine Za Kibongo.
Nakubaliana na wale ambao siku hiyo watatumia kuwapongeza ndugu zao wazazi wao na wapenzi wao. Swali la kujiuliza hapa “tuna adhimisha” ama “tunasheherekea” Valentine?kama tuna adhimisha siku hii, lazima ujue unachoadhimisha, kipi kati yapo juu unachoadhimisha?kama unasheherekea unashehereka nini?otherwise tunakuwa busy na sikukuu tusiyoijua.

Ukitaka lawama valentine we usinunue zawadi, usimtoe mtu dinner, jikaushe kama jumanne zingine tu za kawaida. Kwa Mtazamo wangu mdogo nimebaini “Valentine Day” Wanawake ndo wako excited nayo kuliko Wanaume. Kwanini?Kwa wale wanaume wasio waaminifu siku hiyo wengi hu opt kupumzika nyumbani ili kuondoa lawama. How?Unajua wanaume wengi ndio wanao cheat sasa anapotaka kwenda outing anajua msala unaweza kutokea. Ila kwa wale wanao tazamia kusheherekea ama kuadhimisha siku hii kwa namna yoyote ile basi nina wasiwasi wa baadhi ya watu kukimbiwa kidizaini siku hii, na wengi pasipo kujua kuwa kuna roho nyuma yake watajikuta wakiadhimisha kwa ngono kama ishara ya upendo kumbe ni ile ibada ya kipagani tuliyoisoma hapo juu. Abiria chunga mzigo wako kwenye Valentine.

Swali la Kujiuliza Kuna madhara yoyote ya Mkristo kusheherekea Sikukuu Ya Valentine?

SPECIAL THANKS TO SAM SASALI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!