Saturday 14 February 2015

RAIA WA INDIA JELA MIAKA MITATU

RAIA wa India, Santnam Singh (43) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh 380,000 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kisu katika Uwanja wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNIA).

Hata hivyo, Singh alikubali kulipa faini hiyo na kuachiwa huru katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Akisoma hukumu hiyo leo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma amesema kwamba mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo kutokana na kukiri kutenda kosa hilo hivyo atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh 380,000.
Vile vile  upande wa mashitaka ulithibitisha mashitaka yake bila ya kuacha shaka kwa kutoa kielelezo cha mashitaka hayo ambacho ni kisu.
Awali, Wakili wa Serikali, Anunciatha Leopold alidai kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali ndipo mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo.
Kutokana na hali hiyo, ndipo mahakama hiyo ilipoamua kutoa hukumu dhidi ya mshtakiwa huyo.
Katika utetezi wake, Singh alidai kwamba anategemewa na familia yake na kwamba anaomba apunguziwe adhabu. Ombi hilo lilitupiliwa mbali na kupewa adhabu hiyo.
Leopold alidai kwamba upande wa mashitaka haukuwa na kumbukumbu ya makosa ya nyuma hivyo mshitakiwa ahukumiwe ili iwe fundisho kwa wengine.
Katika kesi ya msingi, Singh alidawa kwamba Januari 10 mwaka huu, maeneo ya Uwanja wa Kimataifa wa Julias Nyerere, alikutwa na kisu kinyume na sheria ya nchi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!