
Kuna mtu wangu wa karibu yuko Iringa ameniambia kuwa kuna Mtoto aliyepatikana asubuhi ya leo akiwa amefungiwa ndani ya nyumba (haijafahamika mara moja kuwa ndiko anako ishi au la!)kwa miaka miwili katika eneo la Kihesa Iringa.
Amesema mtoto huyo alifungwa kwa kutumia mnyororo na kufungwa kwenye kitanda cha chuma.......msichana wa kazi muhusika wa tukio.
Mtoa taarifa hajaweza kudodosa kuwa mtoto anamiaka mingapi na baadhi ya facts ambazo zinaweza kuwepo kwenye hii taarifa, ameweza kunitumia picha tu.
Mwenye taarifa zaidi juu ya hili tukio tunaomba atusaidie tafadhali.
CHANZO: JMF













No comments:
Post a Comment