Wednesday 11 February 2015

MKATE ULIOPAKWA MAYAI NA NDIZI MBIVU

Mkate uliopakwa mayai na ndizi mbivu
Mkate uliopakwa mayai na ndizi mbivu



Mahitaji
  • Mkate vipande  4
  • Mayai 2
  • Maziwa vijiko 6 vya chakula
  • Ndizi mbivu 1 kubwa iliyopondwa
  • Butter vijiko 3 vya chakula (mafuta yoyote yakupikia)
DSC02772
Njia
1.Ponda ndizi kwakutumia umma, zisiwe laini sana
2.Katika bakuli piga mayai  na maziwa.kisha mimina kwenye saani pana iliyojichimba
3.Weka kikaango jikoni na mafuta nusu kijiko,wakati yanapata moto.Chukua kipande kimoja cha mkate,weka kwenye mayai na loanisha  pande zote mbili kisha weka kwenye mafuta yaliyopata moti.
4.Weka ndizi juu ya mkate ulioko jikoni, sambaza vizuri.Chukua kipande chapili cha mkate,weka kwenye mayai na kiloane pande zote mbili kama ule wakwanza,kisha weka juu ya mkate wenye ndizi.Gandamiza kidogo ili mikate ishikane. Geuza na weka mafuta kidogo ili kuivisha mkate wa juu .Mkate tayari kwa kula.
  •  Kaanga mkate kwa moto mdogo ,moto ukiwa mkali mkate hautaiva ndani
  • Fanya haraka unapoweka ndizi na kuloanisha mkate wa pili,ukifanya taratibu uwezekano wa kuunguza kipande cha kwanza unakua mkubwa.
Fanya hivi kwa vipande vyote.
Unaweza kutumia kitafunwa hiki kwaajili ya kifungua kinywa au chai ya jioni.
SPECIAL THANKS TO TOLLYS KITCHEN.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!