Monday 23 February 2015

MICHEZO: ARSENAL WATINGA TATU BORA

image


*Man United maumivu makali
Wakati Arsenal wakishinda na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL),Manchester United wameangukia nafasi ya nne baada ya kupoteza mechi.
Arsenal waliwapiga Crystal Palace 2-1 kwenye mechi kali ugenini, ambapo walipata mabao kupitia kwa penati ya Santi Cazorla dakika ya nane baada ya Danny Welbeck kuchezewa vibaya na Olivier Giroud dakika ya 45.
Ushindi huu wa Arsenal ni wa nane katika mechi tisa, lakini katika dakika za mwisho Palace waliwatisha, ikadhaniwa kwamba wangeweza kusawazisha. Bao la wenyeji lilifungwa na Pape Souare akisahihisha makosa yake ya awali ya kumwangusha Welbeck na kusababisha penati.
Palace walitawala zaidi mchezo huo, ambapo waliingia dimbani wakiwa na rekodi nzuri ya kufungwa mechi moja tu kati ya saba zilizopita, na ushindi wa mwisho dhidi ya The Gunners ulikuwa 1994 kwenye dimba la Highbury , ambapo matokeo yalikuwa 2-1.
MANCHESTER UNITED WAANGUKIA PUA
diver
Katika mechi nyingine wikiendi hii, Manchester United walipoteza kwa 2-1 mbele ya Swansea, wakiwa wamepoteza mechi ya pili kati ya 20 zilizopita, ambapo mshambuliaji wake, Robin van Persie aliumiua na kutokewa nje kwa machela.
Mabao ya washindi yalitiwa kimiani na Ki Sung-yueng kutokana na majalo ya Jonjo na jingine liliufungwa na Bafetimbi Gomis wakati Man U walipata bao kupitia kwa Ander Herrera. Kushindwa huko kumewaangusha United hadi nafasi ya nne.
Kwenye mechi ya kwanza msimu huu Swansea waliwapiga United 2-0 kwenye uwanja wa Old Trafford, wakimpa wakati mgumu kocha Louis van Gaal.
image
Katika mechi nyingine Tottenham Hotspur walikwenda sare ya 2-2 na West Ham kama ilivyokuwa kwa Everton dhidi ya Leicester huku Southampton wakipigwa 2-0 na Liverpool.
Aston Villa wameendeleza mdororo kwa kufungwa 2-1 na Stoke, Chelsea wakaenda sare ya 1-1 na Burnley, Hull wakawashinda Queen Park Rangers 2-1, Sunderland wakaenda suluhu na West Bromwich Albion na Manchester City wakawakiung’uta Newcastle 5-0.
Msimamo wa ligi unaonesha kwamba Chelsea wanaongoza kwa pointi 60 wakifuatiwa na City wenye 55, Arsenal 48 na Man U 47. Southampton wanafuatia nafasi ya tano, nyuma yao wakiwapo Liverpool, Spurs, West Ham, Swansea na Stoke wanafunga 10 bora kwa pointi 36.
Mkiani wapo Burnley wenye pointi 22 sawa na Villa wakati nafasi ya 20 in
CHANZO TANZANIA SPORTS

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!