Monday 23 February 2015

MAMA SALMA KIKWETE AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA MUASISI WA ASP NA CCM BIBI ASHURA ABEID FARAJI HUKO CHAKE CHAKE PEMBA.‏



Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akipokewa na Bi Ashura, mmoja wa wajukuu wa Muasisi wa vyama vya Afro Shiraz na CCM, Marehemu Bibi Ashura Abeid Faraji  mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu eneo la Tibirizi huko Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 21.2.2015. Mama Salma alikwenda nyumbani hapo kuhani msiba wa Muasisi huyo aliyefariki dunia tarehe 27 Novemba 2014. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Ndugu Hanuna Ibrahim Masoud.


Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa Mama Salma Kikwete akiwafariji familia ya Marehemu Bibi Ashura Abeid Faraji aliyewahi kuwa Muasisi wa Vyama vya Afro Shiraz na CCM na piaaliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mbunge kwa nyakati tofauti. Mama Salma alienda nyumbani kwa marehemu huko Tibirizi Chake Chake tarehe 21.2.2015.

PICHA NA JOHN  LUKUWI.  

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!