Tuesday 10 February 2015

IRAN: UPASUAJI NDIO NJIA SULUHU YA UBIKIRA

Mahnaz alikuwa na umri wa miaka 21 alipopatwa na ajali Kaskazini mwa Iran. Na siku hiyo hiyo ya ajali alimpoteza kakake na dadake ajalini,na alipoteza usichana wake pia .


Anasema nililazwa hospitalini.nilipata ajali mbaya sana mfupa wa nyonga yangu ulivunjika .nilikuwa na maumivu makali,na hapo hapo mama yangu akawataka madaktari waangalie kama bikira yangu ipo.
Mahnaz anaelezea kisanga hicho, kwamba siku ambayo mamake alipoamuru uana wari wangu uchunguzwe,mara mtaalamu wa masuala ya sheria za kitabibu kutoka Iranian legal medicine organisation (ILMO) akaja.Na baada ya uchunguzi wakatupa barua iliyoeleza kwamba nimepoteza usichana wangu ajalini.
UMUHIMU WA BIKIRA
Nchini Iran sula la binti kuwa bikira ni muhimu kwa walio wengi,pamoja na mabadiliko makubwa yaliyoikumba jamii ya Irani. Na hii inahusisha upande wa dini na utamaduni,familia zinahitaji kuona binti ana usichana wake kabla ya ndoa.
Katika Jamhuri ya Kiislam mapenzi kabla ya ndoa sio swala la kawaida.Ali Khameni ni kiongozi mkuu nchini Irani na pia ni shehe mkuu wa madhehebu ya Shia,mara kwa mara amekuwa akizungumzia umuhimu wa kiongozi mkuu wa kuwa na usafi wa moyo kama tumu ya uislam na pia suala la kulinda usichana wa binti kama sifa ya uadilifu .
Kuwa mwanamwari sio swala tu la kidini nchini Irani ni suala la mila na utamaduni.binti ambaye ni mwanamwari hapaswi kuolewa bila ya kupata ruhusa ya babake.
UPIMAJI
Kwa binti mwenye asili ya nchini Irani ili athibitishwe kuwa ni mwanamwari bado, girl to be considered a virgin,sehemu zake za siri shurti ziwe zimebana na ndicho madaktari wa kutoka ILMO wanachotazama .
Hakuna takwimu sahihi ambazo zinaweza kutueleza juu ya ukawaida wa suala hili la uchunguzi wa uanamwari wa binti ,lakini ni suala muhimu na haki ya wa wanaharakati na kila wakati wanalizungumzia na hata wanaohusika na masuala ya jamii ndio kipaumbele chao.
Uchunguzi wa namna hii katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku,lakini nchini Irani hakuna sheria mahsusi kuhusiana na suala hili.Ingawa baadhi ya mahakama hufikia wakati wakataka ufanyike uchunguzi wa uanawari wa msichana hasa katika kesi za ubakaji ama mume akilalamika kuwa mkewe si mwanamwari usiku wa harusi yao.
Wakati mwingine ndgu wa bi harusi ama bi harusi mwenyewe huamua kufanya upimaji huo,katika suala kama hili wazazi wa bi harusi hupeleka barua kwenye familia ya mwanaume kama ishara ya kumthibitisha binti yao kuwa bado ni mwanamwari kabla ya harusi ,na kama harusi itaingia dosari ya kuwa waongo,wazazi wa mwanamke hawana cha kujitetea na lawama zote hubebeshwa bi harusi kuwa si mwaminifu.
UBIKIRA TENA
Sima ni binti wa Ki Irani na alifanyiwa vipimo kabla ya ndoa yake ,ingawa yeye hakuwa radhi kufanyiwa kipimo hicho,lakini familia yake ilimlazimisha.mama alikuwa akilia kila siku, naye babangu alikuwa na hasira namie,basi nikalazimika kufanya kipimo hicho ,mamangu akawapa barua familia ya pili na kuwaambia binti yangu hana tatizo bado mwanamwari .
Hata hivyo,baadhi ya wasichana wa Ki Irani wamepata njia mbadala ya upimaji huo,wao huamamua kufanya mapenzi kabla ya ndoa na pindi wakiamua kuolewa na mtu wasiyefahamiana ambaye ni chaguo la familia,hivyo huamua kurejesha uanawari wao kwa njia ya upasuaji mdogo,ambao huchukua muda wa nusu saa.
Dr. Elmi, ambaye ni daktari wa magonjwa ya wanawake nchini Tehran, anasema tunaweza kumgundua msichana aliyefanyiwa upasuaji ili kurejesha uanawari wake,lakini huwa hatusemi kwasababu ni suala nyeti kwa baadhi ya familia .
Binti Sanaz alifanyiwa upasuaji huu miaka mitatu iliyopita.yeye anasema alilelewa na familia ya kidini,ingawa yeye anahitaji kuishi kwa uhuru wa kuamua juu ya mwili wake ,lakini kwa familia yangu ni haramu .Na pindi nilipokuwa na mpenzi,tulifanya kila tulilotaka lakini hatukuoana,nay eye ndiye aliyenitafutia mtaalamu na kunifanyia upasuaji.Nikaolewa mwaka mmoja baadaye na mume alijuwa kuwa mimi nilikuwa mwanamwari .
Somaieh naye alifanyiwa upasuaji huo. Anasema kwamba tofauti ya binti na kijana ni hii kijana anaweza kufanya mapenzi atakavyo na kisha hutafuta mwanamwari wa kuoa.hata sisi wasichana tunatamani kufanya mapenzi kabla ya ndoa , lakini tumepata njia mbadala, upasuaji na sisi tutafanya mapenzi kama wao na kisha baadaye tutarejesha uanawari wetu,kama uanawari wanaona ni muhimu sana kwao
BBC SWAHILI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!