Friday 27 February 2015

HUYU KIJANA ALITAKA KUUZA FIGO KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA

Hekaheka Feb26
Hali ya maisha imekuwa ngumu kwa kijana huyu Abdallah Omar umri wake ni miaka 17, ana kipaji cha uandishi wa script za movie, akapata nafasi kukutana na Geah Habib wa ‘Leo Tena’ @CloudsFM ambaye alimkutanisha pia kijana huyu na Zamaradi Mketema ambaye anafanya show inayohusu movie, “Take One” kwenye Clouds TV.


Baadaye kijana huyu alimtafuta tena Geah na kumuelezea matatizo yake ya kifamilia hali ambayo ilimfanya aamue kuuza figo yake ili aweze kukabiliana na changamoto alizonazo.
Kijana huyo amesimulia kwamba aliwahi kwenda Hospitali ya Amana na kuonana na daktari, baada ya kumueleza nia yake ya kuuza figo daktari alimweleza matatizo ambayo yangeweza kumpata kijana huyo akitoa figo yake kwa umri wake.
Timu ya ‘Leo Tena’ imemuahidi kumsaidia kijana huyo kumkutanisha na watu walio kwenye industry ya movie ili atumie talent yake ya uandishi wa script kupata kipato badala
 ya kuuza figo.

CRD: MILLARDAYO.COM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!