Thursday 19 February 2015

HAYAKUHUSU! MZEE YUSUPH KUOA MKE WA TATU


Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni.



Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani.
Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
Mzee Yusuph akiwa na mke wake pili,Chiku.
Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao.
‘’Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,’alisema Mzee Yusuph.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!