Sunday 15 February 2015

FAHAMU FAIDA 10 Z UKWAJU


Unatakiwa ujaribu kuweka
ukwaju karibu katika kila mlo
wako kwa kila siku kwasababu
ukwaju una faida nyingi kiafya
ambazo hakika zitakufanya uwe
na afya njema au kukuimarisha
afya yako kiujumla



Watu waishio bara la Asia,
Carribian na America ya kusini
wanajua kuwa kula ukwaju
maana yake ni Afya Njema.


Ukwaju unaoliwaa katika maeneo
haya maeneo hayo una faida
nyingi kwa watu wanaoula.

Kwa hiyo siku nyingine unapoenda
kufanya manunuzi ya vyakula
hakikisha unanunua na ukwaju.
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia
ambalo limefungwa na kasha
gumu.

Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani
yake kuna mbegu nyeusi.
Vifundo
hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na
faida za kiafya za ukwaju. Ukwaju
una ladha faluni ya uchachu
ukiwa bado mchanga, lakini kadiri
unavyozidi kukomaa unakuwa na
ladha tamu. Ingawa ukwaju
unakuwa na utamu kadiri
unavyokuwa na kukomaa,
kiujumla ukwaju ni mchachu.

Katika nchi kama Jamaica, Mexico,
Aruba na India, ukwaju
unachanganjwa na sukari na
kuuzwa kama pipi katika mitaa na
madukani. Kula ukwajua au
bidhaa zitokanazo na ukwaju
kuna faida sana. Ukwaju umejaa
Vitamini, fiber, potassium,
magnesium na virutubisho
vingine muhimu kwa afya njema.

Lakini kati ya faida zingine nyingi
za virutubisho na kiafya za
ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni
za muhimu zaidi, na ni kama
zifuatazo:
1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha
antioxidants ambazo zinasaidia
kupigana na saratani. Ukwaju
una carotenes, Vitamini C,
flavanoids na vitamin B zote.

2. Ukwaju unakuepeusha na
ukosefu wa Vitamini C.

3. Ukwaju unasaidia kupunguza
homa na kukupa ulinzi dhidi ya
mafua.

4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha
chakula tumboni.

5. Ukwaju unakusaidia kutibu
matatizo ya nyongo.

6. Juisi ya ukwaju hutumika kama
kitu cha kustarehesha mwili.
7. Ukwaju unapunguza
cholesterol mwilini.

8. Ukwaju unasaidia kuwa na
moyo wenye afya njema.
9. Ukwaju ukiunywa unasaidia
kupooza koo.

10. Ukwaju ukiupaka kwenye
ngozi unasaidia kutibu uvimbe
Kwa Tanzania ukwaju
unapatikana kwenye masoko
karibu yote. 

Manyandahealthy
inakushauri kutengeneza juisi ya
ukwaju nyumbani kwako na weka
sukari kidogo na juisi hiyo iwe
sehemu ya chakula chako. Kama
wewe unapenda kula hotelini au
kwenye vioski basi agizo juisi ya
ukwaju ikusaidi kushushia
chakula.  

Via-Manyanda Healthy.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!