Tuesday, 24 February 2015

Dk. Bilal: Watoto 897,913 wanaishi mazingira hatarishi.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amesema watoto zaidi ya 897,913 nchini wanaishi kwenye mazingira hatarishi na wanakabiliwa na ukatili mbalimbali.


 Akizungumza jana kwenye kongamano la kitaifa la watoto walio katika mazingira hatarishi, Dk. Bilal alisema matatizo ya janga la Ukimwi, umasikini, migogoro ya kijamii, ukatili na unyanyasaji yamechangia ongezeko la watoto walio kwenye mazingira hatarishi. 
Alisema taarifa nyingine zinaonyesha kuwa watoto milioni 2.5 wamekuwa yatima baada ya wazazi wao kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi wakati watoto wa kike watu kati ya 10 wamebainika kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18.
“Hali ya watoto wetu nchini hairidhishi, kwa kuwa watoto wengi na hasa wale walio katika mazingira hatarishi wanakumbwa na vidokezo vya hatari katika umri mdogo,” alisema. 
Dk. Bilal aliongeza kuwa: “Vidokezo hivyo ni pamoja na afya duni, lishe duni na malezi duni, ndani ya familia au kaya na watoto kukaa mitaani ambako wana hatari kubwa ya kubakwa, kupigwa, kutumikishwa.”
Hata hivyo, alisema serikali inafanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wadau kukabiliana na tatizo hilo.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Tanzania, Devocatus Kamara, alisema matatizo yanayowakabili watoto yanahitaji juhudi za wadau wote na kwamba, shirika hilo limekuwa likizifundisha kaya maskini mbinu za kujipatia kipato ili kujiimarisha kiuchumi.
Alisema shirika lake limekuwa likiwasaidia wananchi hao kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa ambavyo kwa ujumla vipo 2,261 ambavyo mbali ya kutunza fedha, vinazalisha na kuuza pamoja mazao yake.
Alisema vikundi vingine 1,000 vya uzalishaji na uuzaji wa pamoja vimeweza kuwasaidia watoto 64,000 walio katika mazingira hatarishi.
“Inawezekana kabisa kila kaya kutunza watoto walio katika mazingira hatarishi, tusiiachie serikali peke yake,” alisema.
Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kujenga uwezo wa kitaalamu kwa maofisa ustawi wa jamii, kuanzisha na kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa watoto walio mazingira hatarishi, kukusanya takwimu za watoto hao na kutoa msaada wa kisheria kwa watoto

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!